Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Novemba 04, 2013

RASTAFARIANMaana alisi ya neno RASTAFARIAN :ni imani ya mtu mweusi au mweupe inayotetea UTU wa MTU MWEUSI.MPIGANIA HAKI YA MTU MWEUSI huitwa RASTAMAN au RASTAWOMAN na kwa WATOTO wao huitwa RASTABABY. 

Imani ya Rasta ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kundi kubwa la waafrika waliokuwa mikononi mwa wakoloni walipoweza kuingia kwenye imani hiyo huku nchi ya JAMAICA ikiwa na wafuasi wengi. Dredy locks ni moja kati ya kitambulisho kikubwa cha Rastafarian,,lakini si kila mwenye dredy locks basi akawa Rastafarian kwani asilimia 25 ya Rastafarian hawana Dredy locks na ndipo tunapoona kwamba kufuga dredy si kuwa na imani ya Rasta bali matendo humpeleka mtu kwenye imani ya Rasta. 

Rastaman hupenda kujiajiri na kufanya shuhguli zake kwa kutumia mikono na si vifaa vya kazi na kati ya kazi za Rasta ni SANAA,, wao hufanya aina zote za sanaa lakini kazi zote hizi Rasta hujiajiri na si kuajiriwa. 

Moja kati ya nguzo za Rastaman ni UPENDO na AMANI,,Rasta hujaribu kutafuta amani popote ipatikanapo, tabia hiyo ya Rast imewafanya Rasta kuheshimiwa popote pale waingiapo lakini baadhi ya jamii huwa tofauti na imani hii. 

 Imani ya Rasta haina chimbuko isipokuwa chimbuko lake ni pale haki ya mtu mweusi ilipo potea na hatimaye jamii kubwa ya watu weusi kutafuta njia ya kutetea utu huo wa mtu mweusi. GABRIEL HAIRE SELASIE aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Ethiopia ni moja kati ya watu waliochangia kukuza imani ya Rasta ulimwenguni na ndipo jumuiya ya Rastafariani ilipoamua kumteua kuwa kiongozi wa Rastafarian ulimwenguni. 

Rasta hutumia muda wa mapumziko kwa kusikiliza burudani ya nyimbo walizo zitunga ambazo nyingi ya nyimbo hizo huwa za kuwapa moyo na kuwafariji watu weusi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni