Kama ilivyoainiwa na Shirikisho la Teknolojia ya habari ya Marekani (ITAA), ni "utafiti, urasimu, uendeleshaji, utekelezaji, usaidizi au usimamizi wa mifumo ya habari hasa ala za programu na vifaa vya kompyuta." IT inahusika na matumizi ya kompyuta zitumiazo umeme na programu za kompyuta kubadili, kuhifadhi, kulinda, kuchecheta, kueneza, na usalama katika kupokea habari.
Leo, neno habari limezunguka nyanja nyingi za kompyuta na teknolojia, na neno hili limekuwa maarufu sana. Wataalamu wa IT hutekeleza jukumu mbalimbali kutoka kuweka ala hadi kubuni mitandao tata ya kompyuta na hifadhidata. Machache kati ya wajibu ya wataalamu wa IT ni kufanya usimamizi wa data, kujumuisha kompyuta ili kutengeneza mtandao, uhandisi wa hifadhidata na programu na vilevile usimamizi na utawala wa mfumo mzima.
Wakati kompyuta na teknolojia za mawasiliano zinapounganishwa, matokeo ni teknolojia ya habari, au "infotech". Teknolojia ya habari ni neno la jumla linaloelezea teknolojia yoyote ambayo husaidia katika kuzalisha, kuendesha, kuhifadhi, kuwasilisha, na / au kusambaza habari. Kwa makadirio, wakati tunapozungumza kuhusu teknolojia ya habari (IT) kama ujumla, ni bainisho kuwa matumizi ya kompyuta na habari yanashirikiana.
Katika siku za majuzi ABET na ACM wameshirikiana kuunda kanuni za akredishon na mitaala ya shahada katika teknolojia ya habari kama uwanja wa masomo uliotofautiana na Sayansi ya kompyuta na pia mifumo ya habari. SIGITE ni kikundi cha kazi cha ACM kilichopewa jukumu la kuweka kanuni hizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni