Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Januari 28, 2013

Teknolojia ya habari


Kama ilivyoainiwa na Shirikisho la Teknolojia ya habari ya Marekani (ITAA), ni "utafiti, urasimu, uendeleshaji, utekelezaji, usaidizi au usimamizi wa mifumo ya habari hasa ala za programu na vifaa vya kompyuta."  IT inahusika na matumizi ya kompyuta zitumiazo umeme na programu za kompyuta kubadili, kuhifadhi, kulinda, kuchecheta, kueneza, na usalama katika kupokea habari.

Leo, neno habari limezunguka nyanja nyingi za kompyuta na teknolojia, na neno hili limekuwa maarufu sana. Wataalamu wa IT hutekeleza jukumu mbalimbali kutoka kuweka ala hadi kubuni mitandao tata ya kompyuta na hifadhidata. Machache kati ya wajibu ya wataalamu wa IT ni kufanya usimamizi wa data, kujumuisha kompyuta ili kutengeneza mtandao, uhandisi wa hifadhidata na programu na vilevile usimamizi na utawala wa mfumo mzima.

Wakati kompyuta na teknolojia za mawasiliano zinapounganishwa, matokeo ni teknolojia ya habari, au "infotech". Teknolojia ya habari ni neno la jumla linaloelezea teknolojia yoyote ambayo husaidia katika kuzalisha, kuendesha, kuhifadhi, kuwasilisha, na / au kusambaza habari. Kwa makadirio, wakati tunapozungumza kuhusu teknolojia ya habari (IT) kama ujumla, ni bainisho kuwa matumizi ya kompyuta na habari yanashirikiana.

Katika siku za majuzi ABET na ACM wameshirikiana kuunda kanuni za akredishon na mitaala ya shahada katika teknolojia ya habari kama uwanja wa masomo uliotofautiana na Sayansi ya kompyuta na pia mifumo ya habari. SIGITE ni kikundi cha kazi cha ACM kilichopewa jukumu la kuweka kanuni hizi.

MSISITIZO WA TAMKO KUHUSU HUDUMA ZA AFYA LA KANISA LA WAADVETISTA WA SABATO



KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO – TANZANIA UNION MISSION

Mkutano wa Mwisho wa Mwaka Uliofanyika tarehe 21 na 22 Novemba, 2012

MSISITIZO WA TAMKO KUHUSU HUDUMA ZA AFYA LA KANISA LA WAADVETISTA WA SABATO LILILOPITISHWA MWAKA 2009, Silver spring, Maryland, USA

Kwa kuwa Kanisa la Waadventista wa Sabato limejitoa kwa dhati kuzingatia ukweli, haki, uhuru, busara, na usahihi katika uendeshaji wa mipango yake yote,

Na Kwa kuwa utoaji wa huduma za afya unapaswa kuaminiwa na umma kwa kutokuingiza mgongano wa maslahi binafsi na majukumu ya kitaalam,

Na kwa kuwa kuna watu walioanzisha huduma za kile kinachoitwa mfumo wa Tiba Mbadala ambao hauendani na ujumbe wa afya wa Kanisa la Waadventista wa Sabato,

Na kwa kuwa Kanisa la Waadventista wa Sabato halina kile kinachoitwa Tiba Mbadala, vyuo vya tiba mbadala, wataalam wa tiba mbadala na mfumo wa tiba mbadala kama ambavyo imekuwa ikitumiwa na wale wanaodai kutumia mfumo huo wa tiba kwa kunukuu maandiko ya Ellen G. White huku wakiwakatisha tamaa watu kwenda hospitali isipokuwa kwenye vituo walivyoanzisha kama sanitariam,

IMEPITISHWA:
Kusisitiza tamko lililopitishwa katika baraza la mwisho wa mwaka 2009 la Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato kule Silver Spring, Maryland, USA linasomeka hivi:

“Kanisa la Waadventista wa Sabato linatamka kwa dhati sharti na shabaha ya Huduma ya Afya inayolenga katika kufanikisha ustawi wa washiriki wake na jumuia inayohudumiwa, na kuboresha afya duniani kwa ujumla.

Kanisa la Waadventista wa Sabato - Makao Makuu - linarudia tena kutoa ahadi yake kwa kanuni ya hadhi ya utu na usawa, haki ya jamii, uhuru, kujitawala, uwezekano wa kupata chakula na maji safi, na uwezekano wa kila mtu kuifikia huduma ya afya iliyopo bila ubaguzi. Kupitia huduma yake ya kuhubiri, kufundisha, kuponya na kuwafanya watu kuwa wanafunzi (discipling), Kanisa linatafuta kuwakilisha utume wa Yesu Kristo kwa namna itakayowafanya waonekane:

>>Kuheshimika ulimwenguni kama wanaofundisha mfano wa ushuhuda timilifu (evidence based) uliojengeka katika kuishi kwa kufuata kanuni za afya katika huduma ya afya ya msingi.

>>Kuonekana wanaaminika wakati wote, huku wakihusiana na mashirika mengine kwa namna ya uwazi wakiwa na malengo na maono yenye ulinganifu katika jitihada za kupunguza maumivu na kushughulikia afya ya msingi na ustawi.

>>Kutambuliwa kwa upeo wake usio na masharti wa kuwakubali wote wanaotafuta afya hii ya msingi na ustawi.

>>Kuhusika sio tu kiutawala, bali pia kiutendaji katika ngazi zote pamoja na kila kusanyiko na washiriki wa Kanisa katika huduma hii ya Afya na Uponyaji.

Na Ieleweke pia kuwa, wale wote wanaojishughulisha na Tiba Mbadala hawawakilishi filosofia ya Kanisa la Waadventista wa Sabato kuhusu Huduma ya Afya isipokuwa wanafanya hivyo kwa manufaa yao wenyewe.

Maoni ya mtoa taarifa: Nyongeza ya “Kuwafanya Wanafunzi (discipling)” inaweza kueleweka vizuri katika kazi ya afya kama Kunasihi (mentoring)

Jumapili, Januari 27, 2013

Morning Star Television (MSTV) in TANZANIA



Tunapenda kutambulisha  Logo ya Morning Star Tv
Hata Hivyo kama unamaoni tofauti usisite kututumia nasi tutayazingatia na kama kuna mtu anaalternative logo badala ya hii au anadhani kuna maboresho zaidi kwa logo hii, tafadhali tutumie wazo lako likiwa katika PSD format na ulitume kwa mazara@morningstartv.or.tz pia unaweza kuwasilisha ofisini kwetu Mikocheni B lilipo kanisa la Waadventista wasabato Ushindi ama Morning Star Radio.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Morning Star Television, yazindua mapango wake wa uchangiaji huko Mwanza na Morogoro.
Je wajua kwa kuchangia uanzishwaji wa MSTV, utawezesha watu Milioni 5 Kufikiwa kwa siku ambapo ingehitaji zaidi ya makanisa 2000
Je wajua, ukitunza kuanzia leo TSH 500 toka kwenye Vocha za simu yako utaweza kuichangia MSTV kiasi kisichopungua TSH 20,000 tarehe 2 March na Hivyo Kuvuka Goli kwa 100% ?
Je wajua kama mshiriki akichangia angalau TSH 10,000 tutaweza kufikia na kuvuka lengo la kuanzishwa MSTV...?





-------------------------------------------------------------------------------------------------------
Sasa unaweza kuchangia ujenzi wa kituo cha Televisheni ya Morning Star, MSTV kupitia
AIRTEL MONEY                                          0686 977 711,
M-PESA                                                         0755 476 266 na pia
TIGO PESA                                                   0655 977 719.

Pia unaweza kuchangia kupitia NBC A/C      0261 0100 2126,
Jina la account TANZANIA ADVENTIST MEDIA CENTER
-------------------------------------------------------------------------------------------------------
Anza leo kukusanya sadaka yako kwa jili ya kufikisha ujumbe kwa watu wote maana kilele cha zoezi hili ni Hapo tarehe 2 March 2013.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------

Kwa maelezo zaidi tembelea H A P A

ENDELEA KUCHANGIA