Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Julai 18, 2012

YALIYO YA KUKUMBUKA


Rudolf II 
 Alizaliwa 18 Julai, 1552 na kufariki 20 Januari, 1612 alikuwa Kaizari wa Dola la Ujerumani kuanzia 12 Oktoba, 1576 hadi kifo chake. Alimfuata baba yake, Maximilian II, na kufuatiwa na mdogo wake, Matthias.


Hendrik Antoon Lorentz 
 Alizaliwa 18 Julai, 1853 na kufariki 4 Februari, 1928 alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi. Alitafiti nadharia ya elektroni. Pia alichunguza nadharia ya Albert Einstein (Relativity Theory) na ya kwanta. Mwaka wa 1902, pamoja na Pieter Zeeman alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.


Nelson Rolihlahla Mandela 
alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918. Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya Apartheid katika Afrika Kusini. Mandela alitumikia kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.


Roald Hoffmann 
Alizaliwa 18 Julai, 1937 alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani akiwa amezaliwa nchini Poland. Hasa alichunguza utaratibu wa athari za kikemia. Mwaka wa 1981, pamoja na Kenichi Fukui alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.


Hartmut Michel 
Alizaliwa 18 Julai, 1948. Ni mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza ugandishaji wa protini. Mwaka wa 1988, pamoja na Johann Deisenhofer na Robert Huber alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.


Joseph Nestroy Kizito 
Amezaliwa 27 Julai, 1982 Uganda ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nichini Uganda, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya FK Vojvodona nchini Serbia tangu Januari mwaka 2005. Yeye pia ndio kapteni wa Timu ya Taifa ya Uganda. Kizito alifunga goli dhidi ya wa pinzani wao wa kuu FK Crevena Zvezda katika Ligi kuu ya Serbia katika msimu wa mwaka 2005/2006 mechi hiyo ilichezeka nyumbani kwao. Goli hilo lilivunja rekodi ya kukaa muda mrefu bila kuwafunga wapinzani wao wa jadi FK Crvena Zvezda zaidi ya miaka kumi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni