Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Julai 15, 2012

Je Unafahamu Kwamba Muziki ni TIBA?
Leo ktk kipindi Morning Star Radio nimeona nikuletee jambo muhimu sana ambalo weeengi walikuwa hawafahamu. Ni suala ambalo hata wewe ukitumia muda wako kuchunguza utabaini ukweli ulio ukweli halisi.


Usikilizaji wa muziki huweza kuwasaidia wagonjwa walio na matatizo sugu ya mkandamizo wa mawazo (stress) na tiba ya kiwango fulani kwa maradhi ya moyo pale mishipa ya moyo inapoelekea kuziba. Utafiti wa kitiba uliofanyika nchini Marekani umebaini kuwa kusikiliza muziki uliotulia unaweza kupunguza ongezeko la msukumo mkubwa wa damu na kuchanganyikiwa kwa wagonjwa wa moyo.

Wataalamu hao wanasema kuwa kuishi huku ukiwa na matatizo ya moyo ni jambo linalosumbua sana kwahiyo hali hiyo inahitaji tiba mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri wa matumzi ya vyakula, vinywaji , lakini pia kuufanya ubongo usipate mkandamizo bila sababu.Lakini hata hivyo Dr. Joke Bradt wa kituo cha sanaa na ubora wa maisha katika kituo cha utafiti wa kitiba katika Chuo Kikuu huko Philadelphia nchini Marekani anasema ‘majaribio yaliyokwisha fanyika ni machache na hasa aina ya muziki unaofaa ni kwamba usikilizwe kwa muda gani na kwamba bado wanalifanyia kazi suala hilo. Tafiti zilizokwisha fanyika ni 23 kwa wagonjwa 1,461 kwa kuwapatia muziki maalum uliorekodiwa na kuungwa katika mishipa , na kazi hiyo hufanywa na wataalamu mabingwa wa masuala ya maradhi ya moyo na sanaa.

Tayari wanamuziki duniani kila mtu anakuna kichwa kufikiria kitu gani atunge na kukiweka katika muziki mororo ili uteuliwe kuwa ‘dawa’ na bila shaka atakuwa billionea ghafla. Penda kusikiliza muziki laini unapojikuta umetindikiwa na mawazo kibao…

Maoni 1 :

  1. Kaka hiyo ni kweli kabisi.muziki sio tu nidawa ya magojwa ya kimwili bali musiki wa injili ni dawa kubwa kwa magojwa ya kiroho. watu ambao wametanga mbali na MUNGU au kukata tamaa wanaposikiliza muziki unao mtukuza MUNGU.wanapona kabisa. lakini Muziki wakidunia nilaana kubwa sana kwani huleta magojwa makubwa ya kiroho. Muziki ukitumiwa vizuri ni BARAKA KUBWA SANA. Lakini ukitumiwa vibaya NILAANA YA AJABU

    JibuFuta