Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Machi 25, 2012

Historia...Karne ya 20


Karne ya 20 ni karne iliyoanzia Januari mosi ya mwaka 1901 na kuishia tarehe 31 ya mwezi Desemba mwaka 2000. Matukio mengi yalitokea wakati wa karne ya ishirini yakiwemo ya kuwa na vita kuu mbili za dunia na kuongezeka kwa sekta ya viwanda duniani. Katika karne hii ya 20 idadi ya watu iliongezeka zaidi ulimwenguni, kuliko karne zote zilizopita.

VITA
Vita Kuu ya Dunia ni jina kwa ajili ya vita inayohusu nchi nyingi katika sehemu mbalimbali za dunia badala ya eneo la nchi kadhaa pekee. Kwa kawaida vita mbili za karne ya 20 huitwa "Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia" (1914-1918) na "Vita Kuu ya Pili ya Dunia" (1939-1945).

Jina hili limepatikana tangu mwanzo wa karne ya 20 katika miaka kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ilipoonekana ya kwamba vita ikianzishwa ingehusu sehemu kubwa ya dunia kutokana na mapatano kati ya mataifa makubwa ya Ulaya yaliyotawala nchi nyingi duniani chini ya mfumo wa ukoloni.

Wanahistoria wengine hudai ya kwamba hali halisi vita kuu ya kwanza ilizohusu dunia yote ilikuwa vita ya miaka saba (1756-1763) kati ya Uingereza na madola ya Kijerumani ya Uprusi na Hannover dhidi ya Ufaransa, Urusi, Austria, Sweden, Saksonia na Hispania. Mapigano yalitokea Ulaya, Amerika ya Kaskazini, Visiwa vya Karibi, India, Asia ya Mashariki, Afrika na baharini kote duniani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni