Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Agosti 10, 2011

Sherehe Za Siku Ya Kuzaliwa Zilivyoanza.



Utamaduni wa sherehe ya kuzaliwa ulianza bara la Ulaya miaka mingi iliyopita. Ilikuwa ikiogopewa kwamba mashetani walivutiwa zaidi kwa watu katika siku zao za kuzaliwa. Ili kuwalinda na madhara, ndugu na marafiki huja kwa mtu mwenye birthday yake wakiwa na mawazo na maombi mazuri. Kupeana zawadi kunaleta furaha/uchangamfu zaidi na kuwafukuza mashetani hao. Hivi ndivyo sherehe za siku ya kuzaliwa zilivyoanza



Mwanzoni ilikuwa ni wafalme tu ndio walioonekana ni umuhimu kwao kuwa na sherehe za siku ya kuzaliwa (inawezekana hivi ndivyo desturi ya mataji yanayovaliwa katika birthday ilivyoanza?). Kadri muda ulivyopita, watoto nao walishirikishwa katika sherehe hizi. Sherehe za mwanzo za birthday za watoto zilikuwa zikifanyika Ujerumani na ziliitwa Kinderefeste.

Wagiriki waliamini kuwa kila mtu ana nguvu za kiroho zinazomlinda na pia mashetani wanaohudhuria wakati wa kuzaliwa kwake na kumuangalia muda wote wa maisha yake. Nguvu hizi za kiroho zina uhusiano wa kiroho na mungu wa siku ambayo mtu huyo amezaliwa.



Warumi pia wanakubaliana na mawazo hayo. Mawazo hayo yaliletwa na imani za wakristo kuwa zinaendana na fikira za watawa wao na watukufu mbalimbali. Desturi ya kuwasha mishumaa juu ya keki imeanza kwa wagiriki. Keki za asali za duara kuashiria mwezi na viwashio pamoja na mishumaa viliwekwa katika sehemu maalum ya mahekalu ya (Artemis). Mishumaa ya birthday, imani za kijadi, zina hadhi maalumu isiyo ya kawaida ya kukubaliwa kwa maombi. Kuwasha mishumaa na moto wa muhanga umekuwa na athari maalum za kiroho tokea pale mtu alipoiweka mara ya kwanza kwa ajili ya mungu wake. Kwa hivyo mishumaa ya birthday ni heshima na ina faida kubwa katika kumpatia bahati njema mtoto mwenye kuzaliwa siku hiyo.



ANAVYOSEMA MUBELWA BANDIO:

Nashukuru kwa UMOJA uliopo (ule chanya na hasi) na
Kwa Baba na Mama, Baba na Mama wakubwa na wadogo, Wajomba na Mashangazi, Mabinamu, Kaka na Dada zangu (wote wakubwa na wadogo), ndugu wote wa hiari na marafiki mnaonifanya NIKUE, nawapenda sana.
Nililojifunza maishani ni kuwa KILA MTU ANA FUNZO, KILA MTU NI SHULE NA KILA MTU NI MUHIMU. Hata kama shule hiyo ni kukufunza usichotakiwa kufanya. Nawapenda sana, nawathamini na nawaheshimu mno. Ninyi kwangu ni sehemu kubwa ya mimi, na SIFA na LAWAMA zote zije kwenu.
NIWE MUWAZI NA MKWELI. Maisha ya sasa yasingekuwa yalivyo bila msaada mkubwa wa wapendwa wangu wakuu wawili. Mke wangu Mpenzi Esther na mwanangu Paulina. NAWAPENDA na NAWAHESHIMU mno. Nina kila sababu ya kujivunia kuwa nanyi. Nakumbuka na kurejea taswira za awali maishani.

MWISHO:
Kila la kheri ktk siku yako ya kuzaliwa Baba Paulina!

Rafiki yangu mmoja alipokuwa mdogo alikuwa anamuuliza mama yake kuwa sisi tunapozaliwa tunatoka wapi mama huyu akawa anajibu eti tunapatikana baharini, rafiki yangu huyo akawa anafahamu hivyo. Alipokuwa mkubwa ujuavyo dunia ilivyo shule akaelewa kuwa kumbe tunazaliwa ndani ya matumbo ya mama zetu na ni kazi kubwa sana kujifungua.
KILA MMOJA AMETOKA MBALI.

Maoni 1 :