Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Mei 24, 2011

SAYANSI NA UNAJIMU....WILIAM SHAO

SIKU MOJA NILIPITA KATIKA BLGO YA KAKA WILIAM SHAO NIKAKUTA MADA AMBAYO ILINIFANYA NIFIKIRI SANA. KUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA SAYANSI NA UNAJIMU? HILI LILIKUWA CHAPISHO LA MWAKA 2007.

http://wshao.blogspot.com/2007/02/kuna-uhusiano-wowote-kati-ya-sayansi-na.html


Unajimu (wakati mwingine pia: astrolojia) ni mafundisho juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha hapa duniani. Wafuasi wa unajimu hutangaza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa.

Kuna aina nyingi za unajimu:

  • wengine wanataka kugundua mwendo wa dunia na utabiri wa mambo yajayo
  • wengine wanaamini ya kwamba tabia za mwanadamu zinatokana na hali ya nyota wakati wa kuzaliwa kwake
  • wengine wanaona nyota kama alama za miungu au nguvu za mbinguni.

Unajimu ni tofauti na astronomia ingawa zote mbili zilianza na kuendelea pamoja kwa karne nyingi. Tangu mwanzo wa sayansi ya kisasa wataalamu walitambua tabia za nyota kuwa magimba ya angani yenye sifa za kifizikia sio pepo, roho au miungu zinazoweza kutawala dunia au wanadamu. Kwa hiyo njia za unajimu (astrolojia) na astronomia zimeachana tangu karne kadhaa.

Tangu mwanzo wa historia wanadamu katika sehemu mbalimbali za dunia walitazama nyota wakitambua nyota zinaonekana tofauti na mwendo wa majira. Walitambua pia uhusiano kati ya kuonekana kwa nyota mbalimbali na kutokea kwa mambo yaliyo muhimu kwa maisha ya kibinadamu.

Kwa mfano kuonekana kwa nyota fulani (hii inategemea mahali duniani) inaweza kuwa alama ya kwamba mvua ni karibu, au majira ya baridi inaanza. Sababu yake ni ya kwamba nyota huonekana kwa vipindi fulani wa mwaka tu; wakati wa miezi mingine zingeonekana wakati wa mchana ambako nuru ya jua inaficha nyota zote hazionekani tena. Masaa za usiku kuna vipindi ambako nyota fulani zinaonekana vizuri angani juu kabisa na kwa njia hiyo zinaweza kutambuliwa kama ishara za majira.


Watu wa kale walikuwa hodari sana kutazama nyota na kutambua mabadiliko yao katika mwendo wa wakati. Hali hii haieleweki kirahisi na watu wa leo waliozoea nuru ya taa za umeme wakitumia wakati wa usiku kutazama TV au kompyuta. Lakini kwa watu wa kale -jinsi ilivyo hadi leo kwa watu wengi vijijini au porini- nyota na mwezi zilikuwa taa hasa wakati wa usiku.

Uhusiano ulioonekana kati ya mabadiliko ya nyota na mabadiliko ya majira yalianzisha elimu ya kalenda pamoja na elimu ya unajimu na astronomia.

Kwa wazee hawa ilionekana kama nyota fulani inatawala majira, hali ya hewa na hivyo maisha ya kibinadamu kwa sababu maisha ya jamii yalitegemea majira na mwendo wa mvua, ukame, baridi au joto. Hapo ni asili ya kuziangalia nyota kama miungu au pepo zenye uwezo fulani. Hasa tabia ya hali ya hewa ya kuchelewa au kuwahi kidogo ilijenga imani ya kwamba kuchelewa kwa mvua ni dalili ya hasira ya mungu yule anayeonekana kama nyota fulani.

Horoskopi

Kati ya mbinu za unajimu zinazojulikana sana duniani ni horoskopi. Chini ya vichwa kama "Nyota zinasema" magazeti mengi huchapisha namna za utabiri wa kila wiki kwa watu kufuatana na tarehe zao za kuzaliwa.

Sayansi



Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli zilizo bainishwa pasi kuthibitishwa.

Aina Za Sayansi

Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika:

Sayansi Asili k.m.

Sayansi Umbile k.m.

Sayansi Jamii k.m.

Sayansi Tumizi k.m.

Pia, kuna sayansi zinahusu mada mbalimbali:

Msingi wa sayansi ni vitendo.

Vitendo vya Kisayansi vina njia zake zinazotumikia kusimamisha kweli ya kisayansi.

Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka Nadharia ama Udhanifu. Halafu tena ili Kweli ikubalike; hutoka kwenye udhanifu; kwa kupitia kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.

Kwa hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaumba nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Isipokuwa kweli watakanusha nadharia hii. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa ni nadharia inayokubalika.

Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kuwa pingifu ya Hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika Jiwe (Maada Yabisi) kuna uvungu ( dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.

Historia

Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmoja mmoja; lakini kadri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wakujitenga. hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo ilionekana kama ni shauku la mtu mmoja mmoja kama awali.

Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa ni sehemu ya historia ya Sayansi. Majina na sifa kutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.

Sayansi na Jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.

Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.

Ingawaje haibanishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maisha ya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu kimamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi.

Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu kuwa mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.

Na hivyo roho ya uchunguzi ndio iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.


…..NA KATIKA MTANDAO WA:

http://www.bibleinfo.com/sw/topics/unajimu-kutafsiri-nyota

Unaeleza kuhusu Unajimu, kutafsiri nyota

Je? Mungu anasema nini kuhusu wao wanao tafsiri nyota kuweza kujua jinsi maisha yao yatakavyokuwa? Imo katika Biblia, Isaya 47:13-15 "Umechoka kwa wingi wa mashauri yako basi nawasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. tazama watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao ndivyo itakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale walio fanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wakukuokoa."

Unajimu ni imani ambayo yafundisha kuwa uwambatano wa mwezi, nyota na jua waweza kuleta tukio katika maisha ya mtu. Katika lugha ya kiebrania neno unajimu ni kutabiri mbingu, kuweza kutoa siri, kutabiri jambo litakalotokea. Imo katika Biblia, Walawi 19:26 "...... Msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi."

Kabla ya wana waisiraeli kuingia katika nchi ya ahadi, walionywa kutofanya unajimu, imo katika Biblia, Torati 18:9, 12, 14 "Utakapokwisha ingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale 12- kwamaana yule atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana Mungu wako anawafukuza mbele yako 14 maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanao shika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe Bwana, Mungu wako, hukupa ruhusa kutenda hayo."

1Samueli 15:23 "Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyongo; kwa kuwa umelikataa neno la Bwana yeye naye amekukataa usiwe mfalme

Wakati mfalme Nebukadreza alipo ota ndoto aliwaita wagana, wachawi, wasihiri na wakaldayo waweze kutafsiri ile ndoto. Imeandikwa Danieli 2:10 "Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme kwa maana hapana mfalme, wala bwana wala liwali aliyetaka neno hili kwa mganga wala kwa mchawi wala kwa mkaldayo."

Imo katika Biblia, Danieli 2:27-28. "Danieli akajibu mbele ya mfalme akasema ili siri aliyoiuliza mfalme; wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu. Lakini yuko mungu mbinguni afunuaye siri naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayo kuwa siku za mwisho."

NITAREJEA KUKUPA DANDOO ZAIDI KUHUSU JAMBO HILI NA NAMNA TULIVYOPOTOSHWA. JE UNAFAHAMU KUWA LIBRARY KUBWA DUNIANI IKO VATCAN KWA PAPA?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni