Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Mei 05, 2011

KATIKA MATENDO YETU

Nilitingwa na jambo ambalo hata hivyo litakuwa na msaada kwa waengi kadri tunavyoendelea kuishi, katika moja ya mambo yaliyonipa wasaa wa kutafakari sana ni pamoja na JINSI MUZIKI UNAVYOANDAA WATU KUELEKEA KATIKA SERIKALI MOJA YA DUNIA. Makampuni ya filamu yanavyotumika. Teknolojia inavyotumika kurahisisha. Hata hivyo ninaandaa utaratibu ambao utatusaidia walau kila wiki kujifunza ama kupata kile nilichopata halafu tuone ni nini tufanye. Kwa kuwa hilo lipo katika mchakato wacha leo nikupe jambo fikirishi.

Kuna wakati nilitakiwa kufanya mahojiano na mkufunzi wa malezi na tabia za vijana na watoto, na ilionekana kuwa inanilazimu kwenda mahali alipo kuwa. Kama ujuavyo kazi za uandishi hasa wa radio mara nyingi huwa tunatumia vifaa maalum vya kuchukulia sauti katika mazingira yoyote. Siku moja betri za kuchaji ninazotumia katika MINI DISC yangu zikawa hazina umeme wa kutosha ikanilazimu kwenda kununua za Panasoniki size ndogo dukani.

Nilishangazwa na bei niliyoikuta, betri 1 tena yakawaida kabisa ila size ndogo inauzwa tsh 450 wakati mara ya mwisho niliuziwa kwa tsh 150 kwa moja. Nikajiuliza ni lini bei hii imepanda hivi: sikupata jibu ila nikachukua jukumu la kuwajulisha marafiki zangu mabadiliko ya bei ya betri niliyoikuta na sio kwa duka moja.

Rafiki yangu mmoja aitwaye JOVIN alinipa changamoto sana aliponiambia kuwa Sio betri pekee…upande wa vyakula pia kuna shida akatolea mfano: Sembe kutoka Tsh 80-100kg mwaka 2000, Tsh 200@kg mwaka 2005, hadi Tsh 9002kg mwaka 2010 Huu ni mfano ambao ni halisi-takwimu.

Lakini pia Kuna mwimbaji mmoja wa kundi linalojihusisha na uimbaji wa MUZIKI WA ACAPPELLA aitwaye MUSA toka SONDA YA DILHU yeye aliniambia kuwa; Nadhani sasa kaka Yusuph umeamini kuwa maisha bora kwa kila mtu ni kwa walioko juu ya madaraka tu. Na hao waishio chini ya dollar moja ni Bora maisha.

Pamoja na kuwa siku hiyo nilipokea msg nyingi toka kwa marafiki na wafanya kazi wenzangu, wacha nimzungumzie DANNY BULENGELA. Mmoja wa watengeneza video za miziki ya injili hapa Tanzania akiwa na studio yake ya ROCK CITY STUDIO alisema: Wakati nasoma msg uliyonituka kaka Yusuph mara umeme ukakatika nikapandwa na hasira zaidi ukizingatia jana yake asubuhi sikusikiliza kipindi radioni kisa nilienda kununua betri ndogo za radio mara baada ya umeme kukatika kama leo kufika dukani naambiwa betri moja ni Tsh 500. Just Imagine nilikuwa katika khali gani.


KATIKA MIZANI, NI UPANDE UPI AMBAO HUWA CHINI?
Maoni 1 :

  1. Ukisoma historia hili jambo ni mpaka WANANCHI wachoke kisawasawa. ZAR wa Urusi alipinduliwa kutokana na haya mambo . Mfalme wa UFARANSA mpaka hakuna tena WAFALME Ufaransa ilikuwa hivihivi mpaka inadaiwa wakati WATU wanakula panya kwa kuwa chakula ghali Mke wa MFALME akawa anadai hivi kama hakuna hata mikate kwanini wasile KEKI? Ikiwa na maana yeye haelewi kuwa kama kwa kawaida KEKI ni ghali kuliko MKATE na ikiwa watu wamefikia kuchoka inamaana hakuna cha keki wala nini!:-(

    JibuFuta