Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Machi 13, 2011

Aibu ya vijana wenye nguvu kulelewa.

------------------------------------------------------------------------------------------------
UHUSIANO ni suala binafsi linalohitaji uamuzi wa mtu husika kwa hiari yake mwenyewe, pengine bila kupangiwa wala kuamuliwa.

-------------------------------------------------------------------------------------------------

Hata hivyo yawezekana ukawapo msukumo kutoka kwa mtu au sababu fulani za msingi na zinazoweza kumfanya mhusika kuingia katika uhusiano huo, pengine kwa kuhitaji kusaidiwa kitu na wala si kwa nia au upendo wa kweli kwa mhusika. Hali hiyo mara nyingi inachangiwa na ukata wa fedha, ambapo si tu wasichana ndio hujikuta wakiingia mikononi mwa wanaume kwa ajili ya kumaliza shida zao, bali siku hizi imekuwa hata wanaume nao wanajirahisisha kwa akina dada au akina mama kwa nia ya kusaidiwa. Hali hiyo ya wanaume kujirahisisha inafahamika zaidi kwa jina la ‘kulelewa’, ikiwa na maana kwamba wanakuwa ni watu wa kulelewa ambapo kwa jina maarufu huitwa ‘Maloo’. Utakuta baadhi ya vijana, hasa wanaoonekana kuwa ni wenye haiba ya mvuto wanakuwa na fikra za kupata akina mama wakubwa au hata wasichana wenye kazi zao ili wapate fedha za matumizi. Vijana hufikia kupangiwa nyumba na pengine hata kupewa magari na wanawake hao ili wayaendeshe. Fikra za kufanya kazi za kutumia nguvu, ikiwa ni pamoja na kujituma katika jua na mvua mara nyingi ni ndogo kwao, kwa kuwa kutokana na ile hali ya ‘ubishoo’ wanayokuwa nayo inawafanya kujiona kuwa ni watu wa gharama na ambao watakutwa na baraka za kupendwa na kulelewa, kwa lugha ya mtaani vijana huita ‘zali la mentali’.

***************************************************************************

Inashangaza zaidi kuona kuwa baadhi yao ni vijana wenye miraba minne, nikiwa na maana wana nguvu na hata uwezo wa kufanya kazi za kutumia nguvu ili waweze kuishi. Wapo wengine ambao angalau hujishughulisha na shughuli za ulinzi wa kumbi mbalimbali za burudani, huku wengine wakijishughulisha na masuala ya uanamitindo.

***************************************************************************

Suala la kijana mwenye nguvu, hasa wa kiume, kutegemea kulelewa kwa asilimia zaidi ya 70 ni hatari, si tu kwa familia zao bali pia kwa taifa zima kiujumla kwa kuwa nguvukazi inapungua. Kulelewa huko kunawafanya kupenda kukaa bila kufanya kazi na tena hasa wakiwa na fikra ya kuwa na maisha bora yenye kila aina ya ufahari, huku wakiwasema vibaya wenzao wanaochakarikia kazi. Mmoja kati ya vijana ambao wanapenda tabia hizo, Michael alipozungumza nami aliniambia haya kwamba wapo wenye kupenda hali hiyo, lakini pia kuna baadhi ya akina mama na akina dada ambao hujipendekeza kwao. Anasisitiza kwamba; ...suala la uhusiano ni la binafsi na linamhusu au kuwahusu watu binafsi na akaongeza kuwa kama akina dada wanatongozwa basi hakuna ubaya kwa wao kama vijana pia kukubali kuwa na akina mama au akina dada wanaowataka. Anafafanua kuwa kukaa bila shughuli muhimu ya kufanya ni kitendo kinachowafanya baadhi ya vijana wa aina hiyo kutegemea zaidi wanawake, hasa wenye fedha nyingi, kwa kuwa mtaji wao unakuwa ni ile hali ya haiba ya mvuto waliyo nayo wao vijana. Anasema kwamba yeye binafsi amewahi kukutana na hali kwamba, mama mmoja mwenye kichele chake cha kutosha, akifanya kazi benki alimtaka. Naye hakuwa na hiyana, akakubaliana naye kwa sababu mwanamama huyo, kwa kuwa suala la fedha za matumizi, hakuwa na tatizo, huku kijana husika akizihitaji. Mwanamama huyo alikuwa ameolewa na mumewe alikuwa ni mtu mzima asiyependa masuala ya ujana. Mwanamama huyo alikuwa na miaka 35, kijana akiwa na miaka 30 wakati mume wa mama huyo alikuwa na miaka 52. Anasema kuwa wakati akiwa na mwanamama huyo tayari yeye alikuwa na mpenziwe mwenye umri wa miaka 24, mwanafunzi tu asiyekuwa na chanzo chochote cha mapato. Anasema kuwa yeye mwenyewe licha ya kila mara kusifiwa na mwanamama huyo kuwa ni kijana mwenye mvuto na kupewa karibu kila alichokihitaji – fedha za matumizi, usafiri na mahitaji muhimu, alihakikisha anakuwa makini. “ Najua unajua tena mwenye kuwa na usawa ni mgumu hali ngumu ya maisha lakini wakati huo huo uelewe kuwa suala la upendo ni muhimu, kwa hiyo mtu akinihitaji mimi sina noma na kwa kuwa ninakuwa makini na uhusiano wangu lakini napata ‘chenji’,” anasema Michael. Pia mwanamama mmoja aliyekubali kuwa na tabia kama hizo za kupenda vijana, Mercy, anasema kuwa kama ilivyo kawaida kwa akina baba watu wazima na waliooa kutembea na wasichana wadogo, ndivyo wao pia huwa na uhusiano na vijana. Anafafanua kuwa ni vigumu kwao kukaa na baadhi ya waume ambao wamejichokea au ambao mara nyingi huwa na kazi nyingine nyingi za kufanya kwa muda mrefu. Anasema kuwa kutokana na uwezo wao wa kifedha, akina mama kama yeye wanaamua kuwarubuni vijana hao na kuwatumia watakavyo, ikiwezekana kuwafungia ndani kabisa. “Ah bwana eh! Kulelewa kulelewa, yaani sisi akina mama tukiwalea hao maloo basi inakuwa ni kosa, tena kubwa? Wao wana haki ya kupendwa na hata sisi kama akina mama tukihitaji vijana basi ni haki yetu kwa kuwa wengine waume zetu wenyewe ni ugonjwa wa moyo,” anasema Mercy. Baba mmoja mwenye umri wa karibu miaka 50 alipata kusimulia jinsi alivyopanda kwenye basi ‘daladala’ jijini Dar es Salaam, na baada ya muda dada aliyekuwa ameketi kando yake kidogo, akiisha kumtazama akachukua simu, akaandika ujumbe halafu akampa ile simu yake. Baada ya bwana huyo kupokea simu kwa mshangao na kuanza kusoma ujumbe, alikuta dada huyo akiwa amemwandikia kwamba amempenda na angependa mwisho wa safari hiyo waende wote wakafanye mapenzi. Baba huyo alimkatalia, akamwambia angependa kwenda lakini hana fedha, na msichana huyo akakata mawasiliano.SWALI:

Maana hao wazazi na wao unaweza kuta wanachaguo lao kwako kwamba yumkini kuna binti waliemuona kuwa atakufaa au wanakwambia oa ktk kabila lako.

Kama kweli mke mwema hutoka kwa Mungu kwa mujibu wa mafundisho ya namna ya kuchagua mchumba tuliyoyapata na neno lake linavyosema, kijana anapopata mwenza mtarajwa/mchumba halafu akawaeleza wazazi, hatmaye wafikie hatua ya wazazi kumkatalia kijana wao.

Je, hilo ni dhihirisho kuwa mke mwema hutoka kwa Mungu?

Maoni 1 :