Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Februari 09, 2011

Hivi Naelewa Kwa Kiasi Gani.

Picha na:
www.
fadhymtanga.blogspot.com

Hii ni hoja nzito mno kuliko unavyoweza kuelewa, hasa kwa kuwa kiasi cha kuelewa si suala la mtu binafsi.

Je, uelewa juu yako binafsi ni wa kiasi gani?

Na je uelewa juu ya nchi yako ni mkubwa kuliko uelewa juu ya nchi jirani?

Picha kwa hisani ya:
http://simon-kitururu.blogspot.com


Tatizo si katika hilo tu, bali je elimu yetu imekuwezesha kuelewa mambo kwa kiasi gani?

Mambo yatakayo kuwezesha kutatua matatizo yako binafsi?

Wakati tukiendelea kutafakari tafakari na ujumbe katika wimbo huu:

MAISHA YANGU NI MLIMA.



Maoni 4 :

  1. huwa tunajua mengi ya nje yetu lakini hatujui chochote kuhusi sisi, hatajitambui

    JibuFuta
  2. Kwa ufupi watu huwa hatujielewi kama tunavyodhani..

    JibuFuta
  3. Ahadi za MUNGU Huwa tunatembea nazo lakini hatujitambui.

    Hivi unataarifa kuwa Mungu hakutupatia roho ya uoga????

    Mungu anaweza kututoa katika hali ya chini na akatuweka ktk hali ya juu...malaki 3:11

    JibuFuta
  4. Ila kuna tatizo pia katika VIPIMO vya BINADAMU!


    KIASI cha kuelewa kama KIPIMO cha kitu huwa nakiogopa sana hasa katika maswala ya KIROHO!

    Kwa kuwa huwa nawasiwasi kuwa labda mbele za MUNGU ,...
    .... adhaniwaye ndiye aelewaye sana KIBINADAMU inaweza kuwa ndio haelewi kabisaa kama kilengwacho ni IMANI!


    Na ukikumbuka pia hata ya dunia,...
    ... kuna wakati walioelewa sana na kuheshimika kuwa wanajua ndio wale waliokuwa wanadai DUNIA iko kama meza na kwa kubisha hilo kanisa KATOLIKI kwa muhuri wa PAPA liliweza kukuua ,...
    ... kitu ambacho twajua siku hizi kuwa DUNIA ni mduara.


    Na hata ukifuatilia historia ya magonjwa ,...
    ... utastukia kuna watu wengi maarufu walikufa kwa KASWENDE na waelewa wa swala waliamini gonjwa hili halina tiba kwa uelewa wake ingawa siku hizi gono na kaswende havimtishi mtu ,...
    ... ingawa ni UKIMWI siku hizi kwa uelewa wa watu ndio hauna tiba,...
    .... kitu ambacho labda vizazi vijavyo vitashangaa ni kwanini watu wengi hivi walikufa kwa UKIMWI kwa kuwa labda wakati huo uelewa wa watu huo utakuwa na jibu rahisi kuhusu UKIMWI mpaka sisi wa kizazi hiki tutaonekana hatujui KUFIKIRIA na hatukuwa na uelewa!


    Nawaza tu kwa sauti!

    JibuFuta