Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Januari 21, 2011

RADIO

Nimefurahi sana, sio leo tu-ni mara nyingi zaidi. Kinachonifanya nifurahi hivyo ni juhudi zako za kupitia mara kwa mara Blog hii...ni kweli hilo limenipa hamasa kubwa kwamba unajali na kuthamini.
Bwana, Mungu akubariki na azidi kukupa Mibaraka hadi ulie machozi ya furaha.

Ngoja nikudokezee lililo moyoni mwangu:
Nina njozi, japokuwa njozi hii kuna ambao wameshaifanya, ILA. Sina hakika kama kwa Tanzania hili jambo limeshafanyika na kama lipo basi halijashamiri kiivyo.

Ninatamani NIWE na INTERNET/BLOG RADIO.
Ambayo licha ya kutangaza kwa kiswahili lakini pia vipindi vyake vingine vitaendeshwa LIVE na vitakuwepo ambavyo vitaruka vikiwa RECORDED.
Nimeona nikwambie jambo hili nikiwa na imani kabisa kwamba utanipa ushauri na njia zipi nipitie ili njozi hii itimie. Ki ukweli zipo RADIO nyingi sana mtandaoni lakini nyingi ya hizo zinarusha matangazo yake kutoka ulaya na chache sana kutoka Afrika hasa Afrika Mashariki, maana wapo wana Afrika Mashariki ambao wapo ughaibuni wameweza kufanya hivyo,. Je, tukiwa Tanzania hapa hapa hatuwezi kwani?
Nitafurahi sana kusikia kutoka kwako MDAU.

Maoni 6 :

  1. Tutaweza tu kwani hakuna kitu kinachoshindikana. na hasa ukiwa na imani na kweli umepania UTAWEZA TU. Mungu yu nawe.

    JibuFuta
  2. KWANI WAO WALIWEZAE MKUU, HATA SISI TUSHINDWE, WAZO ZURI SAAANA, ILA....MMMh labda gharama, mmmh, labda ufundi...mmmh, lakini ulipotoa hoja hii natumai ulishaangalia vikwazo hivi.
    Tupo pamoja mkuu, UTAWEZA KABISA!

    JibuFuta
  3. KWANI WAO WALIWEZAE MKUU, HATA SISI TUSHINDWE, WAZO ZURI SAAANA, ILA....MMMh labda gharama, mmmh, labda ufundi...mmmh, lakini ulipotoa hoja hii natumai ulishaangalia vikwazo hivi.
    Tupo pamoja mkuu, UTAWEZA KABISA!

    JibuFuta
  4. Wow, hili ndilo tumaini letu la leo, wengi husema vijana ni taifa la kesho na wakati maisha yao yanaendelea kwa namna yalivyo katika nchi zao...taifa la kesho kivipi!!??.

    Mambo mengi tunaweza kuyafanya leo leo itakapofika kesho hiyo inayotamkwa yumkini tutakuwa wazee, lipi lingoje lipi.

    Kwa Yasinta Ngonyani na hata kwa Emu-Three Jembe lina maana nyingi ukiamua kuzitafuta hizo japo kiuhalisia lina baki lile lile la kulimia ardhi (shamba)

    Wao wameweza wana nini na sisi tushindwe tuna nini, iweje hivyo.

    NIMEFURAHI NA NINAKUSHUKURU KWA KUNIONESHA USHRIKIANO, TUTAJULISHANA MATOKEO YA DHAMIRA NA NIA.

    MCHAKATO UNAANZIA WAZO LILIPOFIKA KWAKO MDAU.

    JibuFuta
  5. INTERESTING INTRO, MCHARIA!

    Nimefika hapa mara ya kwanza; na nafurahia tu kwamba idadi ya watu wenye ndoto bado ipo palepale hata wasiwe wengi. [YE ARE THE SALT OF THE EARTH- MATTHEW 5:13]

    JibuFuta