Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Julai 11, 2012

William Shakespeare



Waingereza mara nyingi humtazama kuwa ni mwandishi mkuu wa lugha yao. Aliandika hasa maigizo na tamthiliya. Alifanya pia kazi ya uigizaji.
Maigizo yake hupangwa katika vikundi vya
  • michezo tanzia
  • tamthiliya kuchekesha
  • tamthiliya ya kihistoria
Wataalamu wengine hawakubali ya kwamba maandiko yote yanayojulikana kama "Shakespear" yameandikwa na mtu yeye yule. Walio wengi wameridhika ya kwamba huyu Shekespear wa kihistoria mwenyewe alikuwa mwandishi..

William Shakespeare amezaliwa Aprili 1564 - 23 Aprili, 1616 alikuwa mwandishi mashuhuri nchini Uingereza.

Jumatatu, Julai 09, 2012

Kuku wa nyama


Ni aina ya kuku anayefugwa kwa ajili ya nyama. Kuku wa nyama wa kisasa wa biashara, wanaojulikana kwa kawaida kama Cornish crosses au Cornish-bred Rocks huzalishwa kwa wingi, huwa na nyama fanisi na hukua kasi zaidi kuliko kuku wa mayai au kuku wanaotumika kwa zote mbili. Wao wanabainishwa kutokana na ukuaji haraka , uwiano kula ulio juu na viwango vya chini ya shughuli. Kuku wa nyama mara nyingi huwa tayari wafikia uzito wa paundi 4-5 katika wiki nane tu.

Wao wana manyoya meupe na ngozi ya manjano . Kuku hawa wa faida katika nyama kwa sababu inakosa "nywele" za kawaida ambazo wengi wa aina tofauti wanabidi kuchomwa baada ya kutoa manyoya. Kuku wote wa kike na kume huchinjwa kwa ajiliya nyama zao. Katika mwaka wa 2003, kuku wa nyama takriban bilioni 42 walizalishwa,asilimia 80% ambao walitayarishwa na makampuni nne: Aviagen, Cobb-Vantress, Hubbard mashamba, Hybro.

Ilivyoanza

Kabla ya kuanzisha vizao vya nyama (ng'ombe, kuku, nk) kuku wa nyama walikuwa kuku wa kiume (jogoo) ambao hupunguzwa katika shamba la mifugo. Kuku wa walichinjwa kwa ajili ya nyama na wa kike (mwera) waliadhimishwa kwa uzalishaji wa mayai. Ikilinganishwa na leo, nyama ilikuwa chache na ghali ikilinganishwa na mayai, na ilikuwa nyama ya kifahari. Maendeleo ya uzalishaji wa kukumaalum wa nyama ulitenganisha usambazaji wa mahitaji kuku wa mayai kutoka kwa mayai. Hii, pamoja na mafanikio katika lishe na uzalishaji ambako kuliruhusu kuku wa nyama kuzalishwa kila wakati, kulisababisha gharama ya nyama ya kuku kuwa nafuu.

Broilers mara nyingi huitwa "Rock-Cornish," akimaanisha antagandet ya aina ya kuku hybrid zinazozalishwa kutoka msalaba wa kiume wa kawaida breasted Cornish mbili Strain na mwanamke wa tall, boned kubwa Strain wa kizungu Plymouth Rocks.  jaribio hili la kwanza la zao la kuchanganywa la kunyama kuletwa katika 1930s na akawa dominerande katika miaka ya 1960. Kuchanganya huku kwa awali uzazi, ukuaji polepole, na ugonjwa susceptibility, na kuwa na taratibu za kisasa broilers kuwa tofauti sana kutoka Cornish x Rock hybrid.


Mazao na UKisasa Wake

Kuku wa nyama wa sasa ni kizazi tatu (zao la F2 ). Mababu wa kuku hizi za nyama wametoka katika asili nnne tofauti,Wawili ambao wako katika laini ya kiume na wawili ambao wako katika laini ya kike , ambao wanapatana ili kuzaa kuku wa nyama . Uhusiano huu huzuia tabia za kipekee kwa kuwa Matatizo haiwezi tena kusambazwa katika jamii ya kuku wa mayai.  Kwa kuongeza, laini kiume na kike hazizalishwi kwa ajili ya tabia moja;laini ya kike inafaa kuytaga mayai mengi iwezekanavyo , kwani idadi ya mayai yaliyotagwa na kila mwera huchangia katika gharama ya mayai ya kuku wa nyama na hivyo broiler vifaranga vyake. Uwezo wa kutaga mayani chini muhimu katika male Mpya, wakati jogoo uzazi ni muhimu sana.

Kuku wa mayai hulelewa katika mazingira yaliyodhibitiwa pamoja na maelfu ya w vifaranga wenzake. Kuku huyu anapatiwa chakula bila kipimo kupata ambacho ni mlo maalum wenye kiwango cha juu cha protini na hulishwa kutumia mfumo wa kulisha wenye kujiendesha. Hii ni pamoja na hali ya taa bandia inayochochea ukuaji na kwa hivyo uzito wa mwili unaotakikana unafika kwa muda wa wiki 4-8 , kutegemea uzito wa mwili unaotakikana na kiwanda cha kutayarisha nyama. Baada ya kutayarisha, kuku hawa husambazwa kwenye maduka wakiwa freshi au waliohifadhiwa .

Kwa sababu ya ufanisi katika kupata nyama, kuku wa nyama pia ni maarufu katika mashamba ndogo ya familia katika jamii za vijijini, ambapo familia zitalisha kundi ndiogo za kuku hawa.

Kuku hawa wa nyama wakati mwingine hufugwa katika makao ya nyasi kwa kutmbinu mbalimbali inayoitwa pastured kuku, kama ulioendelezwa na Joel Salatin na kukuzwa kwa wazalishaji wa kuku Pastured American Association.

Neno "broiler" ni linajulikana sana katika Amerika ya Kaskazini na Australia lakini siyo mahali pengine katika kuzungumza Kiingereza duniani. Neno "kuku wa mayai" linakutumika sana nchini Pakistan na India, kama ilivyokuwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani zamani na bado sikuhizi katika baadhi ya sehemu ya mashariki ya Ujerumani. Neno hili pia hutumiwa nchini Indonesia, Sweden, Finland, Poland na katika Balkan.

Hoja Yenye Suala la Msingi

Mara nyingi kuku hawa wanaweza kupata matatizo ya miguu kwa sababu miguu yao haiwezi kubeba miili yao mizito. Uchunguzi uliofanywa na Slu Skara (Chuo Kikuu cha Kilimo cha Swedis) ulibaini kuwa tu 1 / 3 ya kuku wa nyama ambao wako karibu kuchinjwa wana afya. Pia, si jambo la kupendeza na hatari kutokan na wanyama wanaokula kuku, na haifai kwa ujumla kufugwa katika mashamba madogo mbalimbali.

Kama taka haifagiliwi katika vyumba hivi na kuzuia kuku hawa kusimama juu ya kinyesi cha Vidonda miguu na Malengelenge yanaweza kutokea. Ndege wanaobadilishwa mara nyingi hawana masuala haya.





Jumapili, Julai 08, 2012

RAISE & SHINE QUARTET


Ni kundi la vijana wadogo linalojihusisha na muziki wa Acappella na linapatikana katika kanisa la Waadventista wasabato Tegeta.

Hapo walikuwa ktk Kipindi Morning Star Radio.

Alhamisi, Julai 05, 2012

MELI



ni chombo kikubwa cha usafiri kwenye maji. Siku hizi meli huwa na bodi ya chumaikisogezwa kwa nguvu ya injini inayochoma diseli. Hadi karneya 19 meli zilijengwa kwa kutumia ubao zikasongezwa hasa kwa nguvu ya upepo kwakutumia tanga. Jahazi ziko hadi leo. Meli hutumiwa hasa kwa kubeba mizigo na abiria. Kuna pia meli za kijeshizinazoitwa manowari. Kuna njia mbalimbali kutofautisha ukubwa wa meli na njia ya kawaida imekuwa tani GTinayotaja mjao wa chombo. Mkuu na kiongozi kwenye meli anaitwa nahodha. Watu wanaofanya kazi kwenyemeli kwa jumla ni mabaharia.

Muundowa meli
  1. Omo ni sehemu ya mbele ya bodi ya meli
  2. Pua la omo linapunguza ukinzani wa maji wakati wa mwendo na kupunguza matumizi ya mafuta ya injini
  3. Nanga hutiwa hadi chini ya maji na kushika meli ikisimama
  4. Bodi ya meli imetengenezwa kwa mabamba ya feleji
  5. Rafadha (au: jembe) ya meli inasogeza chombo mbele ndani ya maji
  6. Tezi (au: shetri) ni sehemu ya nyuma ya meli
  7. Dohani ni faneli au eksosti kwa hewa chafu ya injini
  8. Majengo juu ya sitaha ni kama nyumba kwa ajili ya mabaharia na abiria, huwa pia na chumba cha kutawala meli
  9. Sitaha ni uso wa juu wa meli; ni dari juu ya bodi ya meli; meli kubwa huwa na sitaha mbalimbali chini ya sitaha ya juu

Historia


Vyombo vya usafiri vya kwanza kwenye maji yalikuwa mashua na maboti madogo kama mtumbwi.
Kuanzia mwaka 4000 KK watu wa Misriya Kale wameanza kutengeneza jahazi ndogo. Manmo 1200 KK watu wa Finisia na Ugirikiya Kale walijenga jahazi kubwa zaidi yenye urefu wa mita 30. Wachinawanajulikana walijenga jahazi kuanzia 2000 KK. Waromawa Kale walitengeneza meli iliyobeba watu 1,000.

Katika mazingira ya Mediteranea meli hizi za kwanza zilisogezwa kwa kasia pamoja na tanga. Meli kubwa zakiroma zilikuwa na kasia kubwa zilizopigwa na watumwa wawili au watatu kwa kilakasia.
Jahazi ziliboreshwa hadi kuvuka bahari kuanzia karne ya 15 BK. Wachina naWareno ni watu wa kwanza waliovuka bahari za mbali. Ila tu Wachina baada yakutembelea mara kadhaa pwani za Afrika chini ya Zheng Hemnamo mwaka 1400 waliamua kuacha upelelezi huu lakini Wareno waliendelea kuvukaAfrika na dunia yote na kuanzisha kipindi cha ukoloni cha Ulaya.
Katika karne ya 19 injini ya mvuke ilipatikana hata kwa meli. Melizikawa kubwa zikaendelea kukua wakati injini ya diseli imepatikanakatika karne ya 20.

Aina na idadi ya meli

Bila kuangalia maboti madogo dunianikuna
  • meli za kibiashara 34,882 zenye ukubwa wa tani GT zaidi ya 1,000; jumla ya meli hizi ni tani bilioni 1.04. (mwaka 2007)
    • meli hizi zilibeba jumla ya shehena (mzigo) tani bilioni 7.4 (mwaka 2006) na kiasi hiki kimekuwa asilimia 8 kila mwaka.
    • 37.5% za meli hizi zilibeba shehena ya mafuta
    • 35.8% za meli hizi zilibeba shehena zilizofunguka kama vile madini, makaa mawe, nafaka au simiti
    • 10% zilikuwa meli za kontena
    • 10% ni meli zinazochanganya kila aina ya mizigo
  • manowari 1,240 bila kuhesabu maboti madogo ya kijeshi (mwaka 2002)
    • Marekani ilikuwa na tani milioni 3 za manowari, Urusi na tani milioni 1.35, Uingereza na tani milioni 0.5 na China na tani milioni 0.4.
  • meli za kuvua samaki ni nyingi lakini ziko za kila ukubwa si rahisi kuzipanga. Kuna vyombo 38,400 zenye tani zaidi ya 100. Nyingi zaidi ni ndogo sana; meli kubwa ya kuvua samaki zafikia tani 3,000 halfu kuna meli za viwanda ambako kundi la meli zinapeleka windo la samaki na samaki hizi zinakatwa mara moja na kufungwa tayari kwa kuuzwa madukani zikitunzwa katika barafu.

Ijumaa, Juni 29, 2012

UWEZO WA NENO



“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” 2 Timotheo 3:16-17. Katika Neno la Mungu kimo kila kitu cha muhimu kiwezacho kumkamilisha mtu wa Mungu. Ni kama nyumba ya hazina iliyojaa bidhaa bora sana na za thamani.

“Lenye pumzi ya Mungu,” “ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu” (fungu la 15), na kumfanya mtu wa Mungu, “awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema,” Kitabu hiki kipitacho vitabu vyote kina madai ya juu kabisa kwetu ili tupate kukiangalia kwa kicho. Kukisoma kwa juu juu tu hakuwezi kukidhi [kutosheleza] madai ambayo kinayo juu yetu, wala kutupatia sisi manufaa yanayoahidiwa humo.
 
Tungejitahidi kujifunza maana kamili ya lile Neno la kweli, na kuinywa kwa kina roho ile iliyomo ndani ya Mausia hayo Matakatifu. Kusoma kila siku idadi fulani ya sura, au kukariri kiasi fulani cha Maandiko kilichowekwa , bila kutafakari kwa makini maana ya fungu hilo, kutaleta faida ndogo sana. Kujifunza kifungu cha maneno kimoja mpaka maana yake imekuwa wazi mawazoni mwako, na uhusiano wake kwa mpango ule wa wokovu uwe unaonekana wazi, kuna manufaa sana kuliko kusoma sura nyingi bila kuwa na lengo lo lote linaloeleweka, wala kupata mafundisho yo yote yanayokujenga.

Hatuwezi kupata hekima toka katika Neno la Mungu bila kuwa na bidii ya dhati na maombi katika kujifunza kwetu. Ni kweli kwamba sehemu fulani za Maandiko zi wazi mno kuweza kukosewa; lakini ziko nyingine nyingi ambazo maana yake haiwezi kuonekana upesi kwa kuziangalia kwa haraka, maana ile kweli haiwi juu. Ili kuelewa maana ya vifungu vya maneno kama hivyo, ni lazima kulinganisha andiko na andiko; ni lazima pawepo na utafiti wa makini na kutafakari kwa moyo wa maombi. Kujifunza kama huko kutalipwa maridhawa. Kama mchimba machimbo anavyozigundua tabaka za thamani za madini zilizofichwa chini ya uso wa nchi, ndivyo yule anayeendelea kwa bidii kulichunguza Neno la Mungu kama hazina iliyositirika, atakavyoweza kuziona kweli zile za thamani sana, ambazo zimefichwa kwa mtafutaji mzembe.

Lakini mafundisho hayo matakatifu ya Neno la Mungu usipoyafanya kuwa kanuni na mwongozo wa maisha yako, kweli hiyo itakuwa si kitu kwako. Kweli inafaa tu wakati ule inapotekelezwa kwa matendo katika maisha yako. Kama Neno la Mungu linaishutumu tabia yako moja unayoipenda, hisia yako unayoitunza moyoni mwako, roho uliyoidhihirisha, basi, wewe usigeuke na kumpa kisogo mshauri wako huyo mtakatifu [Neno la Mungu], bali uupe kisogo uovu ule unaoufanya na kumruhusu Yesu kukusafisha na kukutakasa moyo wako. Ungama makosa yako, na kuachana nayo kabisa na kwa nia thabiti, ukiziamini ahadi za Mungu, na kuonyesha imani yako kwa matendo yako. 

Kama kweli za Biblia zinafumwa pamoja na matendo ya maisha yako, basi, zitaweza kuyainua mawazo yako toka katika hali yake ya kuipenda dunia pamoja na upotovu wake. Wale wanaoyajua sana Maandiko watakuwa ni wanaume na wanawake ambao mvuto wao una nguvu ya kuwainua watu. Katika kuzichunguza kweli hizo za Mbinguni zilizofunuliwa, Roho wa Mungu huunganishwa na moyo wako kwa karibu sana. Kuyaelewa mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa huukuza ubongo, huupa mawazo bora, na kuupa nguvu mpya, kwa kuuleta uwezo wake mbalimbali katika mgusano na ile kweli kubwa mno ajabu.

Hakuna somo liwezalo kuupa ubongo nguvu yake na kuiimarisha akili kama kulivyo kujifunza Neno la Mungu. Hakuna kitabu kinginecho chote chenye uwezo mkubwa mno katika kuyaadilisha mawazo, kuupa nguvu uwezo wa akili, kama ilivyo Biblia, ambayo inazo kweli bora kabisa. Kama Neno la Mungu lingesomwa linavyopaswa kusomwa, basi, tungeweza kuuona upana wa mawazo, uthabiti wa nia, ubora wa tabia, kama ule unaoonekana kwa nadra sana katika nyakazi hizi.

Walakini, kujifunza Biblia kunapewa nafasi ya pili katika mawazo yetu, na kwa ajilihiyo, hasara kubwa inapatikana. Ufahamu wetu unafuata usawa wa mambo yale unayoyazoea. Kama wote wangeifanya Biblia kuwa somo lao, tungeweza kuwaona watu waliokua vizuri, wenye uwezo wa kufikiri kwa kina zaidi, ambao wangeonekana kuwa na ujuzi mkubwa kuliko wale waliosoma kwa bidii sayansi mbalimbali pamoja na historia za ulimwengu huu, ambao wanaiacha Biblia. 

Biblia humpa mtafutaji wa ile kweli nidhamu ya hali ya juu kiakili, naye anapotoka katika kutafakari mambo hayo ya Mungu, nguvu zake za akili zikiwa zimesitawishwa; nafsi yake inanyenyekezwa, wakati Mungu na kweli yake iliyofunuliwa kwake inapotukuzwa. Ni kwa sababu watu hawazifahamu historia za thamani zilizo katika Biblia, ndiyo maana kuna hali ya kumtukuza mno mwanadamu na heshima ndogo mno hutolewa kwa Mungu.

Biblia inacho kile kiwezacho kumfanya Mkristo kuwa na nguvu ya kiroho na kiakili. Mtunga Zaburi asema hivi, “Kuyafafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga.” Zaburi 119:130. Biblia ni kitabu cha ajabu. Ni historia inayotufunulia sisi mambo ya karne zile zilizopita. Pasipo kuwa na Biblia, sisi tungekuwa tumeachwa kufuata dhana mbalimbali na hadithi za uongo kwa habari ya matukio ya vizazi vile vilivyopita. Ni unabii unaolifunua pazia la siku zijazo. 

Ni Neno la Mungu, liufunualo mpango ule wa wokovu, ambalo linatuonyesha njia ile ambayo kwayo sisi tunaweza kuikwepa mauti ile ya milele, na kujipatia wema wa milele na uzima wa milele. Katika vitabu vyote vinavyoigharikisha [vinavyoijaza] dunia hii, haidhuru viwe
vya thamani ilioje, Biblia ni Kitabu kipitacho vitabu vyote, inastahili kabisa kuwa somo letu na kupewa heshima. Haitupatii sisi historia ya ulimwengu huu tu, bali maelezo ya ulimwengu ule ujao. Ina mafundisho yahusuyo maajabu ya malimwengu mbalimbali; inatufunulia katika ufahamu wetu tabia ya Mwasisi yule wa mbingu na nchi. Ndani yake umo ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu.

Kuvichunguza vitabu vya falsafa na sayansi hakuwezi kuiletea akili na maadili kile ambacho kujifunza Biblia kunaweza kutuletea, mradi tu kiwekwe katika matendo yetu. Yule anayejifunza Biblia anaongea na wazee wa zamani pamoja na manabii. Anagusana na ile kweli iliyovikwa mavazi ya lugha ya heshima, ambayo ina mvuto wenye nguvu unaoupendeza moyo, na kuyainua mawazo toka katika mambo ya dunia hii kwenda kwenye utukufu ule wa maisha ya baadaye ya milele. Ni hekima gani ya mwanadamu inayoweza kulinganishwa na ufunuo wa utukufu wa Mungu. Mwanadamu mwenye maisha mafupi, asiyemjua Mungu, anajitahidi kuipunguza thamani ya Maandiko, akidai kwamba, maarifa yake ya sayansi anayodhania kuwa anayo, hayawezi kupatana na Neno la Mungu; lakini Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu.

Wale wanaojigamba kwamba wanayo hekima nyingi kuliko ile ifundishwayo katika Neno la Mungu wanahitaji kunywa kwa kina zaidi katika chemchemi hiyo ya maarifa, ili wapate kuuona ujinga wao ulivyo hasa. Wanadamu hujisifu wenyewe kwa hekima waliyo nayo, wakati hekima hiyo ni upumbavu mtupu. Hebu na asiwepo mtu awaye yote anayejidanganya mwenyewe. “Mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. 

Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.” 1 Wakorintho 3:18-19. Ujinga mkubwa mno unaowaletea laana wanadamu hivi sasa ni ujinga wa kukosa kuyajua masharti ya Sheria ya Mungu [Amri Kumi – Kut. 20:3-17] ambayo yanawafunga wanadamu wote; na ujinga huo ni matokeo ya kudharau kulichunguza Neno la Mungu. Ni mpango wake Shetani kuyashughulisha mno mawazo kiasi cha kuwafanya wanadamu kukiacha Kitabu hicho Kikuu cha Mwongozo, na hivyo kuwafanya waongozwe katika njia ile ya uasi [uvunjaji wa Amri Kumi – Yak. 2:10-12] na maangamizi.

Biblia haipewi heshima na kuwekwa mahali pake inapostahili miongoni mwa vitabu vya ulimwengu huu, japokuwa kuisoma kuna umuhimu usio na kifani kwa roho za wanadamu. Katika kuzichunguza kurasa zake mawazo yetu huziona mandhari [picha] zile tukufu za milele. Twamwona Yesu, Mwana wa Mungu, akija katika dunia yetu, na kuingia katika pambano la ajabu ambalo limezivunjilia mbali nguvu zile za giza. Lo! ni ajabu jinsi gani, ni jambo ambalo karibu halisadikiki kabisa kwamba Mungu yule wa milele angeweza kukubali Mwana wake apate kudhalilishwa kiasi kile, ili sisi tupate kuinuliwa juu na kuketi pamoja naye katika kiti chake cha enzi!

 Hebu kila mwanafunzi wa Maandiko na atafakari ukweli huo mkuu, ndipo hatatoka katika kujifunza Biblia pasipo kutakaswa, kuinuliwa juu na kuadilishwa. Ile kweli itafunuliwa akilini mwake na kutumiwa na Roho wa Mungu katika moyo wake. Kwa njia ya kuunganishwa na Mungu, Mkristo atakuwa na mawazo safi na mapana zaidi, yasiyopendelea kufuata maoni yake mwenyewe aliyokuwa nayo hapo kwanza. Uwezo wake wa kupambanua mema na mabaya utapenya ndani zaidi, uwezo wake wa akili utakuwa na uwiano mzuri zaidi.

Akili yake, ikitumika katika kuzitafakari zile kweli tukufu, itapanuka, na katika kujipatia maarifa yale ya mbinguni ataweza kuujua vizuri zaidi udhaifu wake alio nao, naye atakua katika imani na katika unyenyekevu wake wa moyo. Usikivu mdogo tu ukitolewa kwa Neno la Mungu, mashauri ya Mungu huwa hayazingatiwi, maonyo yanayotolewa huwa kazi bure, neema na hekima ya mbinguni haitafutwi ili dhambi zile zilizopita zipate kuepukwa na kila waa la ufisadi lipate kusafishwa katika tabia yetu. Daudi aliomba, akasema, “Unifahamishe njia ya mausia yako [yaani, amri zako – KJV].” “Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika Sheria yao [Amri Kumi].” Zaburi 119:27,18.

Ipo kazi kubwa ya kufanywa na mwanafunzi wa Biblia mwenye bidii; kwa sababu vito vya thamani vya ile kweli vinatakiwa kukusanywa na kuletwa juu, kisha vinapaswa kutengwa mbali na urafiki wo wote na makosa [mafundisho potofu]. Ingawa Biblia ni ufunuo utokao mbinguni, hata hivyo, wengi hawayaelewi mafundisho yake ya mbinguni. Tunapaswa kugundua maono mapya ya ile kweli katika Agano la Kale na Agano Jipya, hatuna budi kukiona kina na upana upitao kiasi wa zile kweli tunazofikiri kwamba tunazijua, lakini ambazo sisi tuna ujuzi wake wa juu juu tu. Yule anayeyachunguza Maandiko kwa bidii ataona kwamba mwafaka upo kati ya sehemu mbalimbali za Biblia; atagundua uhusiano wa kifungu kimoja cha maneno na kile kingine, na thawabu ya taabu yake [ya kujitahidi kukichunguza] itakuwa ya thamani kubwa mno.

Katika eneo lote la ufunuo huo zimetawanyika chemchemi za furaha, amani na shangwe za ile kweli ya mbinguni. Chemchemi hizo za furaha zinaweza kufikiwa na kila mmoja atafutaye. Maneno yale ya Uvuvio, yakifikiriwa sana moyoni, yatakuwa kama vijito vinavyotiririka kutoka katika mto ule wa maji ya uzima. Mwokozi wetu aliomba kwamba akili za wafuasi wake zipate kuzinduliwa ili kuyaelewa Maandiko hayo. Kila tunapojifunza Biblia kwa moyo wa maombi, Roho Mtakatifu huwa karibu nasi kutufunulia maana ya maneno yale tusomayo. 

Mtu yule ambaye akili yake imetiwa nuru kwa kulifafanua Neno la Mungu, hatajisikia tu kuwa anapaswa kutafuta kwa bidii ili apate kulielewa Neno lile, bali kwamba anapaswa kuwa na ujuzi bora wa sayansi zile nyingine. Atajisikia kwamba ameitwa kwa mwito ule mkuu katika Kristo Yesu. Kadiri mwanadamu anavyounganishwa kwa karibu sana na lile Chimbulo la maarifa yote na hekima, ndivyo kadiri atakavyojisikia kwamba hana budi kusonga mbele katika kujipatia mambo yale ya kiakili na kiroho. Roho Mtakatifu, kwa njia ya ile kweli ya Mungu, huuhuisha uwezo ule wa kiroho uliokufa na kuuvuta moyo kuelekea mbinguni.

Basi, chukua Biblia yako na kujiweka mbele za Baba yako wa Mbinguni, ukisema, “Unitie nuru; unifundishe kweli ni nini.” Bwana ataifikiria sala yako, na Roho Mtakatifu ataitia kweli hiyo moyoni mwako. Katika kuyachunguza Maandiko wewe mwenyewe, utakuwa umejiimarisha katika imani. Ni jambo la maana sana kwamba uweke moyoni mwako akiba ya kweli hizo za Mungu. Unaweza kujikuta uko mahali ambako hutapata nafasi ya kukutana na watoto wa Mungu. Unahitaji kuzificha hazina za Neno la Mungu
moyoni mwako, ili upinzani utakapokuja dhidi yako, upate kulipima kila jambo kwa Maandiko hayo.

Kweli ni ya milele, na kupambana kwake na uongo [mafundisho potofu] kutaudhihirisha tu uwezo wake. Kamwe tusikatae kuyachunguza Maandiko pamoja na wale ambao tunayo sababu ya kuamini kwamba wanataka kujua kweli hiyo ni nini. Tuseme ndugu mmoja anashikilia maoni yaliyo tofauti na yako, naye anakuja kwako, na kupendekeza kwamba wewe uketi chini pamoja naye na kulichunguza jambo lile katika nuru ya Maandiko; je! ungesimama ukiwa umejazwa na chuki bila sababu na kuyashutumu mawazo yake, na wakati uo huo ukiwa unakataa kumpa usikivu wako usiopendelea upande wo wote? Njia pekee sahihi kwetu sisi kama Wakristo ingekuwa ni ile ya kuchunguza msimamo uliotolewa katika nuru ya Neno la Mungu, ambalo litaifunua kweli na kuufichua uongo. 

Kuyadhihaki mawazo yake kusingeweza kuudhofisha msimamo wake, ingawa [yale usemayo] yangekuwa ni ya kweli. Hebu kilete kila kitu kwenye Biblia; kwa maana hiyo peke yake ndiyo kanuni ya imani na mafundisho ya dini. Hatuna budi kujifunza ile kweli sisi wenyewe; tusimtegemee mtu awaye yote kufikiri kwa niaba yetu, haidhuru awe ni nani au awe na cheo gani. Hatupaswi kumwangalia mwanadamu ye yote kama kiongozi mkamilifu [asiye na dosari] aliyewekwa kwa ajili yetu. Tunapaswa kushauriana pamoja na kunyenyekeana; lakini wakati uo huo hatuna budi kumwangalia Mungu kwa ajili ya kututia sisi nuru ile ya mbinguni, ili kila mmoja wetu apate kukuza tabia ile itakayoweza kushinda katika jaribio la siku ile kuu.

Sisi tunaishi katika siku za mwisho, wakati makosa [mafundisho ya uongo] yaliyojaa udanganyifu wa hali ya juu yanapokelewa na watu na kusadikiwa, wakati ile kweli [Neno la Mungu – Yn. 17:17] inapotupiliwa mbali. Wengi wanachukuliwa na mkondo wa maji na kuingia katika giza [la ujinga] na ukafiri, wanaikosoa Biblia, wanaleta mavumbuzi ya kishirikina [uchawi], wanaleta nadharia zisizoungwa mkono na Maandiko, pamoja na dhana zinazotokana na falsafa ya kipumbavu; lakini ni jukumu la kila mmoja wetu
kujitahidi kupata ujuzi kamili wa Maandiko. Umuhimu na faida ya kujifunza Biblia haviwezi kusifiwa mno. Katika kuyachunguza Maandiko mawazo yetu huongozwa katika kuifikiria sana ile kafara ya Kristo isiyo na kikomo katika kutupatanisha sisi. Tunapouona upendo wake, tunapotafakari juu ya kujidhili kwake na mateso yake, roho ile ile ya kujikana nafsi na kujitoa mhanga kwa faida ya wengine inaamshwa ndani ya mioyo yetu. Tunapomtazama Yesu kwa jicho la imani, tuta“badilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile utukufu utokao kwa Bwana, aliyeRoho.” 2 Wakorintho 3:18.
 
Na Bibi E. G. White, The Power of the Word, 
...au Kichwa cha makala ya awali ni: “Apples of Gold Library No. 10.”
 
ZINGATIA: Maneno na mafungu ya Biblia yaliyofungiwa ndani ya mabano haya [ ] yameongezwa kwa ufafanuzi tu kwa yule anayetaka kusoma kwa kina au anayeona neno lililotumika pale ni gumu. Wakati wa kusoma unatakiwa kuyaruka, isipokuwa kama yanasaidia kuikamilisha sentensi hiyo.