Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Julai 05, 2012

MELIni chombo kikubwa cha usafiri kwenye maji. Siku hizi meli huwa na bodi ya chumaikisogezwa kwa nguvu ya injini inayochoma diseli. Hadi karneya 19 meli zilijengwa kwa kutumia ubao zikasongezwa hasa kwa nguvu ya upepo kwakutumia tanga. Jahazi ziko hadi leo. Meli hutumiwa hasa kwa kubeba mizigo na abiria. Kuna pia meli za kijeshizinazoitwa manowari. Kuna njia mbalimbali kutofautisha ukubwa wa meli na njia ya kawaida imekuwa tani GTinayotaja mjao wa chombo. Mkuu na kiongozi kwenye meli anaitwa nahodha. Watu wanaofanya kazi kwenyemeli kwa jumla ni mabaharia.

Muundowa meli
 1. Omo ni sehemu ya mbele ya bodi ya meli
 2. Pua la omo linapunguza ukinzani wa maji wakati wa mwendo na kupunguza matumizi ya mafuta ya injini
 3. Nanga hutiwa hadi chini ya maji na kushika meli ikisimama
 4. Bodi ya meli imetengenezwa kwa mabamba ya feleji
 5. Rafadha (au: jembe) ya meli inasogeza chombo mbele ndani ya maji
 6. Tezi (au: shetri) ni sehemu ya nyuma ya meli
 7. Dohani ni faneli au eksosti kwa hewa chafu ya injini
 8. Majengo juu ya sitaha ni kama nyumba kwa ajili ya mabaharia na abiria, huwa pia na chumba cha kutawala meli
 9. Sitaha ni uso wa juu wa meli; ni dari juu ya bodi ya meli; meli kubwa huwa na sitaha mbalimbali chini ya sitaha ya juu

Historia


Vyombo vya usafiri vya kwanza kwenye maji yalikuwa mashua na maboti madogo kama mtumbwi.
Kuanzia mwaka 4000 KK watu wa Misriya Kale wameanza kutengeneza jahazi ndogo. Manmo 1200 KK watu wa Finisia na Ugirikiya Kale walijenga jahazi kubwa zaidi yenye urefu wa mita 30. Wachinawanajulikana walijenga jahazi kuanzia 2000 KK. Waromawa Kale walitengeneza meli iliyobeba watu 1,000.

Katika mazingira ya Mediteranea meli hizi za kwanza zilisogezwa kwa kasia pamoja na tanga. Meli kubwa zakiroma zilikuwa na kasia kubwa zilizopigwa na watumwa wawili au watatu kwa kilakasia.
Jahazi ziliboreshwa hadi kuvuka bahari kuanzia karne ya 15 BK. Wachina naWareno ni watu wa kwanza waliovuka bahari za mbali. Ila tu Wachina baada yakutembelea mara kadhaa pwani za Afrika chini ya Zheng Hemnamo mwaka 1400 waliamua kuacha upelelezi huu lakini Wareno waliendelea kuvukaAfrika na dunia yote na kuanzisha kipindi cha ukoloni cha Ulaya.
Katika karne ya 19 injini ya mvuke ilipatikana hata kwa meli. Melizikawa kubwa zikaendelea kukua wakati injini ya diseli imepatikanakatika karne ya 20.

Aina na idadi ya meli

Bila kuangalia maboti madogo dunianikuna
 • meli za kibiashara 34,882 zenye ukubwa wa tani GT zaidi ya 1,000; jumla ya meli hizi ni tani bilioni 1.04. (mwaka 2007)
  • meli hizi zilibeba jumla ya shehena (mzigo) tani bilioni 7.4 (mwaka 2006) na kiasi hiki kimekuwa asilimia 8 kila mwaka.
  • 37.5% za meli hizi zilibeba shehena ya mafuta
  • 35.8% za meli hizi zilibeba shehena zilizofunguka kama vile madini, makaa mawe, nafaka au simiti
  • 10% zilikuwa meli za kontena
  • 10% ni meli zinazochanganya kila aina ya mizigo
 • manowari 1,240 bila kuhesabu maboti madogo ya kijeshi (mwaka 2002)
  • Marekani ilikuwa na tani milioni 3 za manowari, Urusi na tani milioni 1.35, Uingereza na tani milioni 0.5 na China na tani milioni 0.4.
 • meli za kuvua samaki ni nyingi lakini ziko za kila ukubwa si rahisi kuzipanga. Kuna vyombo 38,400 zenye tani zaidi ya 100. Nyingi zaidi ni ndogo sana; meli kubwa ya kuvua samaki zafikia tani 3,000 halfu kuna meli za viwanda ambako kundi la meli zinapeleka windo la samaki na samaki hizi zinakatwa mara moja na kufungwa tayari kwa kuuzwa madukani zikitunzwa katika barafu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni