Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Juni 06, 2011

TOKENI MIJINI

Itizame picha iliyopo hapo chini kwa makini kabla hujaendelea kusoma maelezo yanayofuatia…STEAL SLAVE!!!!!. Hii ni kazi iliyofanywa na mmoja wa marafiki zangu anayeitwa CELESTINE KIMARO. Kwa ufupi ana mambo meeengi ya kuijulisha, kuikumbusha na kuelimisha Jamii Yetu. Rafiki yangu, au au nikuite “Ndugu” yangu maana pia wewe ni “Msomaji” wangu…(Mtayarishaji). Unaweza, ikiwa utamhitaji mpate na katika facebook kwa jina hilooo...hapo juu.


E. G. White

Msaada kwa Maadili na Usalama wa Jamii

Mkusanyo wa Maandiko ya ELLEN G. WHITE

Mfasiri: M. Mwamalumbili

Country Living - Kiswahili

DIBAJI

Faida za kuishi shamba [vijijini] zimesisitizwa tena na tena katika mashauri yanayotolewa na Roho ya Unabii. Mawingu ya dhoruba yanayojikusanya yanaashiria kwamba yafaa kuanza kupaza sauti ili kutoa wito wa kuihama miji. Ni budi iwe wazi kwa kila Mwadventista Msabato mwenye akili kujua ya kwamba kuishi mjini, pamoja na msongamano wa watu uliopo, vishawishi vyake na migogoro ya vyama vya wafanyakazi inayozidi kuongezeka, hakuweki mazingira yenye kuleta afya kwa familia za Kikristo.

Kwa miaka mingi maelfu ya Waadventista Wasabato wameelekezwa kuchagua mazingira

yanayofaa kuweka makazi yao na katika uhusiano wao na mashirika ya ulimwengu kwa njia ya

mashauri yatokanayo na shuhuda juu ya mambo hayo ya maana sana ambayo yamechapishwa na

kutawanywa katika sehemu nyingi. Ishara mbaya za hatari kubwa iliyo karibu sana kutokea

zinapoonyesha ugumu wa kuzitambua hatari hizo na ukali mno wa pambano lililo mbele yetu,

inaonekana kwetu ya kwamba ni jambo linalofaa kuuchapisha tena ushauri huu kwa kutumia

mtindo huu ambao unaweza kuyanasa mawazo ya kila mshiriki wa kanisa.

Na kwa kufikiria nyakati hizi tulizo nazo [hivi sasa], ni mahali pake, sio tu kurudia ushauri ule

unaofahamika sana uliochapishwa muda mrefu uliopita, bali kuzitilia nguvu semi hizo kwa kuzitoa kwa mafundisho ya kinagaubaga yaliyopata kuchapishwa toka wakati hata wakati katika gazeti la Review and Herald au yaliyoandikwa katika barua zake za ushauri zilizoandikwa kwa watenda kazi waliokabidhiwa madaraka katika kazi ya Mungu. Kitendo kama hicho kinapatana kabisa na maagizo ya Bibi E. G. White kwa wadhamini wake ili waweze kutayarisha "kwa ajili ya kuchapishwa maandiko yangu yaliyokusanywa pamoja kutoka katika maandiko yangu ya mkono," kwa maana, kama alivyosema yeye mwenyewe yana "maagizo aliyonipa Bwana kwa ajili ya watu wake." Mwaka wa kuandikwa au kuchapishwa kwa mara ya kwanza umetolewa pamoja na kumbukumbu ya chanzo cha kila kifungu cha maneno [kilichotumika].

Wito wa dhati uliotolewa katika kijitabu hiki unataka pawepo na nia ya kutekeleza jambo hili,

lakini [kwa wakati uo huo] onyo hili zito linatolewa ili watu wetu wasithubutu kukurupuka

[kufanya mambo bila kufikiri na kupanga vizuri]. Tungependa kuyaelekeza mawazo yenu hasa kwa tahadhari zile zinazopatikana katika Sehemu ya Saba, "Kuongozwa kwa Maongozi ya Mungu," ambayo inatokea kwenye kurasa za . Kijitabu hiki sasa kinawekwa uwanjani kama jibu la msimamo ulioamuliwa na viongozi wa kanisa hili kwamba [sasa] wakati umefika wa kurudia

kusema tena na tena kilio kile cha, "TOKENI MIJINI."

WADHAMINI WA UCHAPISHAJI WA MAANDIKO YA ELLEN G. WHITE

YALIYOMO

Ukurasa

Wito wa Kuihama Miji............................................................. ............................

Kuikwepa Migogoro ya Vyama vya Wafanyakazi................................................

Ombi kwa Wazazi........................................................... ......................................

Kazi Katika Sehemu za Shamba........................................................... .................

Kujiandaa kwa Hatari Itakayoletwa na Amri ya Jumapili.....................................

Kujikusanya Watu Wengi katika Taasisi Zetu za Kazi..........................................

Kuongozwa kwa Maongozi ya Mungu............................................................ .......

Taasisi Zetu za Kazi Kuwa Mbali na Maeneo Yenye Msongamano wa Watu.......

Kukimbia Wakati wa Hali ya Hatari Pambano Litakapokuwa Linafikia Mwisho..

SEHEMU YA KWANZA

Wito wa Kuihama Miji Hatari Kubwa Zilizomo Mijini

Ni wachache wanaotambua umuhimu wa kukwepa, kwa kadiri iwezekanavyo, uhusiano wo wote

ule unaoleta uadui kwa maisha yetu ya kidini. Katika kuchagua mazingira yao, ni wachache mno

wanaoweka mawazoni mwao ufanisi wao wa kiroho katika nafasi ya kwanza.

Wazazi na familia zao hukimbilia mijini, kwa sababu wanadhani kwamba ni rahisi kupata maisha mazuri huko kuliko mashambani [vijijini]. Watoto wao, wakiwa hawana kazi yo yote ya kufanya wasipokuwa shuleni kwao, hujipatia elimu ya mitaani. Kutoka kwa marafiki zao waovu

wanajifunza tabia za uovu na ubadhirifu [utumiaji mbaya wa fedha na vitu].

Wazazi huyaona hayo yote, lakini itahitaji kujitolea mhanga kuweza kuyasahihisha makosa yao hayo, nao [wazazi] huendelea kuishi mahali hapo walipo mpaka Shetani anawatawala watoto wao kabisa. Ni afadhali kujinyima mambo yote na kila tarajio la kidunia kuliko kuzihatirisha roho hizo za thamani mlizokabidhiwa kuzitunza. Watashambuliwa vikali na majaribu, nao yapasa wafundishwe jinsi ya kuyakabili; lakini ni wajibu wenu kuuondolea mbali kila mvuto, kulivunjilia mbali kila zoea, kukata kila kifungo kinachowazuia msiwe na uhuru kamili, ulio wazi, na kujitoa wakf ninyi wenyewe kwa moyo wenu wote pamoja na familia yenu kwa Mungu.

Badala ya msongamano wa watu uliomo mjini, tafuteni mahali fulani palipo kimya [pa upweke]

kwa kadiri iwezekanavyo, mahali palipo salama mbali na majaribu, nanyi mkiwa pale waleeni na

kuwaelimisha ili wapate kuwa watu wenye manufaa katika maisha yao. Nabii Ezekieli ndivyo

anavyoorodhesha sababu zilizoifanya Sodoma kutenda dhambi na kuangamizwa:

"Kiburi, chakula tele, na uvivu mwingi vilikuwa ndani yake pamoja na binti zake [vitongoji vyake]; wala haukuitia nguvu mikono ya maskini na wahitaji." Wale wote wanaotaka kuokoka ili wasipatikane na maangamizi kama yale ya Sodoma, hawana budi kuukwepa mwenendo ule ulioleta hukumu za Mungu juu ya mji ule mwovu." ----- Testimonies, Gombo la 5, uk. 232,233 (1882).

Kuishi Mijini Sio Mpango wa Mungu

Ulimwenguni kote miji inageuka na kuwa mahali penye maovu mengi sana. Kila upande

huonekana mambo machafu na sauti za uovu. Kila mahali kuna vishawishi vya kuamsha ashiki

[tamaa mbaya ya uasherati] na ubadhirifu [matumizi mabaya ya mali na vitu]. Wimbi la rushwa na uhalifu linazidi kuumuka daima. Kila siku inayopita huleta taarifa za kutumia nguvu ----- ujambazi, mauaji, kujiua, na uhalifu mwingine usiostahili hata kutajwa.

Maisha yaliyomo mijini sio maisha halisi, tena ni ya kinafiki. Tamaa kubwa sana ya kupata fedha, mambo ya mpwitompwito [msisimko] yapitayo kasi pamoja na kutafuta anasa, kiu ya kuwakoga [kujionyesha ufahari kwa] wengine, utajiri na ubadhirifu, mambo yote hayo ni nguvu ambazo, kwa sehemu kubwa sana ya wanadamu, huyageuzia mawazo yao mbali na kusudi halisi la maisha yao. Wanaufungua mlango wa kuingiza ndani yao maelfu ya maovu. Kwa vijana mambo hayo yana nguvu nyingi ambayo karibu haizuiliki kabisa.

Mojawapo ya majaribu yaliyojificha sana na ya hatari sana yanayowashambulia mno watoto na

vijana katika miji ni kule kupenda anasa [starehe]. Sikukuu ni nyingi; michezo na mashindano ya

mbio za farasi huwavuta maelfu, na ule mpwitompwito upitao upesi pamoja na anasa huwavuta

kwenda mbali na majukumu mazito ya maisha yao. Fedha ambayo ingetunzwa kwa ajili ya

kuitumia kwa mambo mazuri zaidi hutapanywa ovyo katika burudani zao nyingi.

Kutokana na utendaji wa mashirika ya amana, na matokeo ya vyama vya wafanya kazi na migomo yake, hali ya maisha mjini daima inakuwa ngumu zaidi na zaidi. Taabu kubwa ziko mbele yetu; na kwa familia nyingi kuondoka kwao kutoka mijini kutakuwa ni kwa lazima.

Mazingira ya nje katika miji mara nyingi ni ya hatari kubwa kwa afya. Uwezekano wa kudumu wa kupatwa na magonjwa, kuenea kwa hewa chafu, maji machafu, chakula kilichochafuliwa, majengo yaliyosongamana pamoja yenye giza na yasiyofaa kiafya, ni baadhi ya mambo mabaya ya kukabiliana nayo humo.

Halikuwa kusudi la Mungu kwamba watu waishi kwa kusongamana sana mijini, wakisongamana

pamoja katika mlolongo wa majumba katika kitalu kimoja na katika nyumba za kupangisha zenye vyumba vingi. Hapo mwanzo aliwaweka wazazi wetu wale wa kwanza katikati ya madhari nzuri na sauti nzuri. Anataka sisi tuifurahie siku ya leo. Kadiri tunavyokaribia sana kuwa katika hali ile inayopatana na mpango wa Mungu wa awali, ndivyo kadiri tutakavyokuaa na nafasi nzuri zaidi ya kujipatia afya ya mwili, akili, na roho. ----- The Ministry of Healing, uk. 363-365. (1905)

Moyo wa Kusitasita

Sikuweza kulala baada ya kupita saa nane ya usiku mpaka asubuhi ya leo. Wakati wa usiku

nilikuwa natoa ushauri. Nilikuwa nazisihi baadhi ya familia kutumia njia alizoziweka Mungu, na

kuondoka mijini ili kuwaokoa watoto wao. Wengine walikuwa wanasitasita tu, bila kufanya juhudi yo yote iliyo dhahiri.

Malaika wale wenye rehema walimharakisha Lutu na mkewe na binti zao kwa kuwashika mikono yao. Lutu angekuwa ameharakisha kama Mungu alivyotaka, mke wake asingegeuka na kuwa nguzo ya chumvi. Lutu alikuwa na roho hiyo ya kuchelewa-chelewa [kusitasita] mno. Hebu sisi na tusiwe kama yeye. Sauti ile ile iliyomwonya Lutu kuondoka Sodoma inatuamuru sisi, ikisema, "Tokeni kati yao, mkatengwe nao... Msiguse kitu kilicho kichafu." [2 Kor. 6:17.]

Wale wanaolitii onyo hilo watapata kimbilio. Hebu kila mwanaume na awe macho sana kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, tena ajaribu kuiokoa familia yake. Hebu na ajifunge kibwebwe [mkanda] kwa kazi hiyo. Mungu ataonyesha hatua kwa hatua linalopaswa kufanywa baada ya hapo. Isikilizeni sauti ya Mungu kupitia kwa mtume wake Paulo, isemayo: "Utimizeni wokovu wenu kwa kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema" [Wafilipi 2:12,13]. Lutu akalikanyaga bonde lile tambarare kwa hatua za kujilazimisha na kuchelewa-chelewa tu. Kwa muda mrefu sana alikuwa amezoeana na watenda maovu wale hata hakuweza kuiona hatari kubwa iliyomkabili mpaka hapo mke wake aliposimama katika bonde lile akiwa nguzo ya chumvi milele." ----- Review and Herald, Des. 11, 1900.

Miji Itapatilizwa kwa Hukumu za Mungu Wakati umekaribia ambapo miji mikubwa itapatilizwa kwa hukumu za Mungu. Katika kitambo kidogo tu kilichobaki, miji hiyo itatikiswa vibaya mno. Haidhuru iwe mikubwa kiasi gani au majengo yake yawe imara jinsi gani, haidhuru vifaa vya kujihami na moto viwe vimeandaliwa kwa wingi namna gani, acha Mungu ayaguse majengo hayo, katika muda wa dakika chache tu au saa chache yatakuwa yameharibiwa kabisa na kuwa magofu. Miji hiyo miovu [isiyomcha Mungu] itafagiliwa mbali kwa fagio la maangamizi. Katika uharibifu unaoyapata majengo makubwa na sehemu kubwa za miji hivi sasa, Mungu anatuonyesha kile kitakachoiangukia dunia yote. ----- Testimonies, Gombo la 7, uk. 82,83. (1902).

Matokeo ya Maonyo Yaliyopuuzwa

Nimeagizwa kutangaza ujumbe huu kuwa miji ile iliyojaa maasi [uvunjaji wa sheria], na ile iliyo

miovu kupita kiasi, itaharibiwa kwa matetemeko, kwa moto, na kwa mafuriko. Dunia yote

itaonywa na kujua kwamba yuko Mungu atakayedhihirisha mamlaka yake kama Mungu. Mawakala [wajumbe] wake wasioonekana kwa macho [malaika] watasababisha maangamizi, kuteketeza kwa moto, na vifo. Utajiri wote uliolundikwa utakuwa kama si kitu....

Maafa yatakuja ----- yaani, maafa ya kuogofya mno, yasiyotarajiwa kabisa; na maangamizi hayo yatafuatana moja baada ya jingine. Kama watu watayasikia [watayatendea kazi] maonyo haya ambayo Mungu ametoa, na iwapo makanisa yatatubu, na kurudia utii wao [kwa Mungu], basi, miji mingine itaachwa isiharibiwe kwa muda fulani. Lakini endapo watu waliodanganyika wataendelea kutembea katika njia ile ile walimokuwa wakitembea, wakiendelea kuidharau Sheria ya Mungu [Amri Kumi], na kuhubiri [mafundisho ya] uongo mbele ya watu, basi, Mungu ataruhusu majanga yawapate ili akili zao zipate kuamshwa.

Bwana hatawatupilia mbali kwa ghafula wale wote wanaozivunja amri zake [kumi], wala

kuyaangamiza mataifa mazima; lakini ataiadhibu miji na mahali pale ambapo watu wamejitoa

kabisa kutawaliwa na nguvu za kishetani. Kwa ukali sana miji ya mataifa itashughulikiwa, hata

hivyo haitapatilizwa kwa ghadhabu kali mno ya Mungu, kwa sababu baadhi ya watu waliomo

humo watajinasua kutoka katika madanganyo hayo ya yule adui [Shetani], kisha watatubu na

kuongolewa, na wakati uo huo watu wengi sana watakuwa wanajiwekea akiba ya ghadhabu kwa

siku ile ya ghadhabu [ya Mwana-Kondoo, yaani, Kristo]. [Ufunuo 6:14-17; 15:1; 16:1-21.] -----

Evangelism, uk. 27. (1906)

Ukaribu Sana wa Kuja kwa Hukumu za Mungu

Zipo sababu kwa nini sisi tusijenge [nyumba zetu] mijini. Juu ya miji hii, hukumu za Mungu zi

karibu sana kuiangukia. ----- Letter 158, 1902. Laiti kama watu wa Mungu wangeyajua maangamizi yaliyo karibu sana kuja juu ya maelfu ya miji, ambayo kwa sasa imejisalimisha kabisa kuabudu sanamu [Kol. 3:5,6; Efe. 5:5-7; Kut. 20:4-6]. ----- Review and Herald, Sept. 10, 1903.

Maono ya Maangamizi Makubwa

Alfajiri Ijumaa iliyopita, kabla tu sijaamka usingizini, mandhari [picha] iliyonigusa sana moyoni

ilionyeshwa mbele yangu. Nikajiona kana kwamba nimeamka usingizini, ila sikuwa nyumbani

mwangu. Kupitia katika madirisha niliweza kuona moto mkubwa wa kutisha uliokuwa

unayateketeza majumba. Mipira mikubwa ya moto [huenda ikawa ni mabomu] ilikuwa ikidondoka juu ya nyumba zile, na kutoka katika mipira hiyo mishale ya moto ilikuwa inaruka kuelekea kila upande. Ilikuwa haiwezekani kabisa kuizuia mioto hiyo iliyokuwa imewashwa, tena mahali pengi palikuwa panaharibiwa. Hofu kuu iliyowashika watu ilikuwa haielezeki. ----- Evangelism, uk. 29. (1900)

Juhudi za Mungu za Kuwaamsha Watu

Nikiwa bado ningali pale Loma Linda, California, Aprili 16, 1906, maono ya ajabu sana yalipita

mbele yangu. Wakati wa njozi zangu za usiku, nalikuwa nimesimama kwenye mwinuko [kilima], kutoka hapo niliweza kuziona nyumba zikitikiswa kama tete katika upepo. Majengo, makubwa kwa madogo, yalikuwa yakianguka chini. Majumba ya anasa wanayoyatembelea watu wengi, nyumba za michezo ya kuigiza, hoteli, na nyumba za matajiri zilitikiswa na kuharibiwa kabisa. Maisha mengi yakafutiliwa mbali, na anga ilikuwa imejaa sauti za vilio vikubwa kutokana na wale waliokuwa wamejeruhiwa na kuogofywa sana.

Malaika wa Mungu waangamizao walikuwa wanafanya kazi yao. Mguso mmoja tu, majengo

yaliyojengwa imara sana ambayo watu walifikiri kwamba yalikuwa salama kutokana na hatari ya

kila namna, kwa ghafula yakawa malundo ya takataka. Hapakuwa na hakika ya kuwa na usalama

mahali po pote pale. Mimi sikujiona kuwa nimo katika hatari yo yote maalum, lakini utisho mkuu wa matukio yale yaliyopita mbele yangu mimi siwezi kupata maneno ya kuelezea. Ilionekana kana kwamba uvumilivu wa Mungu ulikuwa umefikia kikomo chake kabisa, na ya kwamba siku ile ya hukumu ilikuwa imekuja.

Malaika yule aliyekuwa amesimama kando yangu ndipo akanipasha habari kwamba ni wachache tu waliokuwa na wazo lo lote kuhusu uovu uliomo katika ulimwengu wetu hivi leo, na hasa uovu ule ulio katika miji mikubwa. Akatangaza kwamba utawala wa Mungu ulio mkuu kuliko wote, na utakatifu wa Sheria yake [Amri Kumi], havina budi kufunuliwa kwa wale wanaoendelea kukataa kutoa utii wao kwa Mfalme huyo wa wafalme. Wale wanaochagua kubaki katika hali yao ya uasi [kuvunja Amri zake Kumi], ni lazima wapatilizwe kwa hukumu kwa rehema [zake Mungu], ili, kama ikiwezekana, wapate kuamshwa [kuzinduliwa] watambue uovu wa njia yao. ----- Testimonies, Gombo la 9, uk. 92,93. (1909)

Hatari Itakayowakabili Watakaoendelea Kubaki Mjini Bila Sababu Kulingana na nuru ile niliyopewa, mimi nawasihi watu kutoka na kuvihama vituo vikubwa vilivyojaa watu wengi. Miji yetu inazidi kuwa miovu, tena, inaonekana wazi zaidi na zaidi ya kwamba wale watakaobaki ndani ya miji hiyo bila sababu [ulazima wo wote] watafanya hivyo kwa athari kubwa ya wokovu wa nafsi zao. ----- Manuscript 115, 1907.

Nimekusudia jambo, hili ndilo fundisho ninalotamani sote tulipate. Nitafanya muendelezo wa machapisho ya kitabu kiitwacho TOKENI MIJINI. Kwa kuzingatia umuhim wa huduma katika jamii…sina budi kukichapisha kitabu chote hapa kwa msaada wa www.swahilitruth.com. FUATANA NAMI.

Jumapili, Juni 05, 2011

MBINU ZA USALAMA

Afya ya mwili, akili na hisia wakati wote huathiriwa na majanga, vurugu, hali ya hewa, chakula, mazingira, matukio ya kila siku na changamoto za

maisha. Utumiaji wa mbinu rahisi za zamani za uponaji zinaweza kutuwezesha kuishi kwa amani na usalama licha ya matukio yanayotuzunguka.

Mazoezi ya Capacitar yafuatayo yanatolewa ili yatumike wakati tunapojisikia kudhoofika, kuwa na wasiwasi au kufadhaika na kuvunjika moyo.

Mbinu hizi ni kwa wote, ama tukiwa tumenusurika katika majanga, tukiwa tunahudumia wengine ama tukiwa tumefunikizwa na msongo wa maisha

ya kila siku. Changamoto ni kuyajenga mazoezi haya kwenye maisha yetu ili yaweze kuwa sehemu ya pili ya asili yetu na yanaweza kutumika

wakati wowote tunapotambua kuwa na msongo, kuishiwa nguvu, hisia za mfadhaiko na kupoteza msimamo. Tafadhali nakili, sambaza na utumie

wewe mwenyewe pamoja na wengine. Mazoezi zaidi pamoja na nadharia yanapatikana kwenye vitabu vya Capacitar au Tovuti: www.capacitar.org.

KAZI YA PUMZI

Pumzi ni chanzo cha uhai, huleta nguvu mpya kwenye mkusanyiko wa seli nwilini na chembechembe za uhai ili kustawisha

mwili, akili na nafsi nzima ya mtu. Tunapotoa pumzi, sumu na msongo uliojikusanya hutoka. Kupumua wakati ukiwa na msongo, ni

njia inayofaa kuachia mahangaiko ambayo hujikusanya mwilini. Kupumua kwa kina katika wakati mgumu kunaweza kubadilisha

kabisa namna tunavyoshughulikia hali fulani. Kazi ya pumzi ikiunganishwa na taswira za mwanga au za vitu vya asili huweza kukuza

hisia za amani, utulivu na makini.

• Kupumua Kwenye Tumbo: Kaa vizuri ukiegemea kiti na ufumbe macho. Pumua kwa kina na ujisimike kwenye muda uliopo, ukiachia

mawazo na mashaka yote. Weka mikono yako kwenye tumbo, pumua kwa kina kupitia pua yako na ufikirie kuwa hewa inatiririka kupitia mwili wako

hadi kwenye kituo ndani ya tumbo lako. Fikiria kuwa tumbo lako linajaa hewa kama vile puto. Shikilia pumzi yako kwa muda mfupi halafu utoe

pumzi pole pole kupitia mdomoni, huku ukikaza misuli ya tumbo lako, ukiachia mahangaiko yote mwilini. Endelea kupumua kwenye tumbo kwa

dakika kadhaa. Mawazo yakikujia, taratibu yaachie, rudi kwenye taswira ya hewa ikipita ndani na nje ya mwili wako.

• Kupumua Katika Vitu Vya Asili: Miti na vitu vya asili ni vyanzo vikubwa sana vya nguvu kwa kutusimika na kutuponya. Vua viatu

vyako, uweke miguu yako juu ya ardhi ( au ufikirie kuwa unafanya hivyo). Pumua kwa kina ukifikiria kuwa miguu yako ni kama mizizi ya mti

inayoingia ardhini. Pumua ndani nguvu ya ardhi kupitia miguu yako na upumue nje msongo, mahangaiko na maumivu.

MAZOEZI YA TAI CHI

Mwondoko wa kubembea:

Simama wima miguu yako ikiwa imeachana usawa wa mabega na mikono yako ikiwa upandeni mwa mwili wako.

Nyanyua visigino vyako wakati viganja vya mikono vikiwa juu, na unyanyue mikono yako mpaka usawa wa kifua chako. Geuza

viganja vyako na ushushe mikono yako chini wakati ukishusha visigino na ukinyanyua vidole vya miguu kwa namna ya mwondoko

wa kubembea. Endelea na mwondoko polepole ukibembea mbele na nyuma huku ukipumua kwa kina. Kwa kila mwondoko

shusha mabega, legeza mikono na vidole vya mikono. Fanya zoezi hili kwa ulaini na taratibu. Pumua kwa kina na uelekeze fikra

kuwa miguu yako imepandwa thabiti kwenye mama Ardhi na vidole vyako vya miguuni vikiwa kama mizizi mirefu ikiunganishwa

na nguvu ya ardhi inayolisha. Ukinyanyua mikono fikiria kuwa una uwezo wa kushusha nguvu ya mbingu ili ikusafishe na kukujaza. Huu mwondoko

ni wa manufaa sana kwa ajili ya athari za majanga ( trauma ) na mfadhaiko.

Manyunyu ya Mwanga:

Mguu wa kushoto ukiwa mbele, nyanyua mikono juu kupita kichwa chako, halafu ishushe kama vile

unajinyunyizia mwanga. Sikia nguvu ikisafisha na kujaza nafsi yako. Rudia upande mwingine, mguu wa

kulia ukiwa mbele. Pumua ukiingiza manyunyu ya mwanga, halafu toa pumzi ukiachia yale yote yasiyofaa

ndani mwako. Sikia mwanga ukikusafisha na kukujenga upya. Zoezi hili ni bora sana kwa watu wenye

mfadhaiko au wanaohangaika na majeraha ya athari za majanga (trauma).

Kuachia yaliyopita na kuwa Wazi Kupokea:

Ukiwa na mguu wa kushoto mbele, viganja vya mikono ukivikunja taratibu vikaangalia chini na mikono ikiwa katika usawa wa

kifua. Sukuma mikono yako nje taratibu kama sehemu ya duara, ukiondoa msongo wote, ubaya, na vurugu ndani mwako.

Geuza viganja kuelekea juu na uvivute kwa nyuma kuelekea kifuani, ukipumua ndani amani na uponaji. Rudia huku mguu wa

kulia ukiwa mbele, pumua, ukitoa nje maumivu na vurugu. Pumua ndani amani na uponaji.

Ruka Hewani:

Mguu wa kushoto ukiwa mbele, mkono wa kushoto ukiwa juu, ogelea au ruka hewani. Mwondoko lazima uwe huru na mwepesi,

mikono na mabega vikiwa vimelegea. Rudia mwondoko upande wa kulia ukianza na mkono wa kulia ukiwa juu. Ruka kwa

uhuru hewani huku ukiachia yote yanayokuelemea, ujisikie mwepesi, hai na huru. Fungua moyo wako kwenye uwezekano wote

katika maisha yako na uponaji. Hii ni njia nzuri kuondoa maumivu kwenye mgongo, mabega na kichwa.

KUSHIKA VIDOLE KWA KUTAWALA HISIA KALI

Zoezi lifuatalo ni njia rahisi ya kushughulikia hisia kwa kushika kila kidole. Hisia ni

kama mawimbi ya nguvu yanayosogea yakipita katika mwili, akili na roho. Katika kila

kidole, kunapita mfereji au meridiani ya nguvu inayounganika na kuhusika na kiungo Fulani na hisia fulani. Hisia kali hufanya nguvu kuziba na kusababisha maumivu au msongamano

mwilini. Kushika kila kidole huku ukipumua kwa kina huweza kuleta uponaji na kuondoa

maumivu.

Kushika vidole ni chombo cha manufaa sana kwa kutumia kila siku ya maisha.

Katika hali ngumu au changamoto ambazo huleta machozi, hasira au wasiwasi, unaweza

kushika vidole ili kuleta amani, makini na utulivu ili mwitikio ufaao au hatua ifaayo ifanyike.

Zoezi linaweza kufanyika pia kama taamuli pamoja na muziki au kufanyika kabla ya kulala

ili kutoa matatizo ya siku nzima na kuleta mburudiko wa kina wa mwili, akili na na roho.

ZOEZI:

Shika kila kidole kwa dakika 2-5. Unaweza kushika

mkono wo wote. Pumua kwa kina, tambua na ukubali hisia

kali inayokusumbua ndani mwako. Toa pumzi polepole

pamoja na hisia hii. Fikiria hisia hii ikitiririka kupitia kidole

chako na kuingia ardhini. Vuta pumzi ndani pamoja na

fahamu ya kuunganika, nguvu na uponaji. Toa pumzi

polepole, ukitoa matatizo na hisia kali za zamani. Mara

nyingi unaposhika kila kidole, unaweza kusikia mapigo

wakati nguvu na hisia zinaposogea na kuwiana.

Unaweza kushika vidole vya mtu mwingine

aliyekasirika au kuchukizwa. Kushika vidole kunasaidia

sana watoto wanolia au waliochukia au kwa watu

wenye woga sana, wenye wasiwasi, wagonjwa au

wanaokufa.


MBINU YA KUWA HURU KUTOKANA NA HISIA KALI - EFT

Mbinu hii iliyokuzwa na Gary Craig, Ph. D ni ya manufaa sana kwa kuzibua na kupona hisia kali,

hofu, wasiwasi, maumivu kutokana na hisia kali, hasira, kumbukumbu za majanga na athari sugu, vile vile

kuondoa dalili za mwili na maumivu kama vile kuumwa kichwa, na maumivu ya mwili kwa ujumla. Mbinu

imejengeka juu ya nadharia ya eneo la nguvu la mwili, akili, roho pamoja na nadharia ya meridiani ya

uganga wa Mashariki. Matatizo, athari za majanga na maumivu huweza kusababisha kuziba katika

mtiririko wa nguvu mwilini. Kupigapiga au kubonyeza pointi za acupressure zinazoungana na mifereji au

meridiani za nguvu huweza kusaidia kusogeza nguvu iliyoziba na kuleta afya ya mtirirko wa nguvu mwilini

na katika eneo la akili. (Gary Flint, Ph.D. Emotional Freedom Technique.)

Zoezi:

1. Fikiria jambo la kushughulikia na upime kiwango chake:

Chagua jambo la kushughulikia, shida, hofu, wasiwasi, kumbukumbu mbaya au kutojisikia vizuri. Kwa

kutumia kipimo cha 0 - 10, pima kiwango cha wasiwasi ulionao kuhusiana na shida yako. Kama ni vigumu kupima

tumia njia ya rahisi ya kuona kama shida ni: kubwa, wastani, ndogo au hakuna.

2. Pigapiga mfuatano wa Pointi za Acupressure mara 7- 9:

Pumua kwa kina na upigepige mara 7 - 9 ukitumia vidole vya shahada na vya kati:

• Nyusi zinapoanzia 1

• Nyusi zinapoishia 2

• Chini ya macho juu ya mfupa 3

• Chini ya pua 4

• Chini ya mdomo 5

• Chini ya kwapa (inchi 4) 6

• Chini ya mtulinga pande mbili za kidari 7

3. Pigapiga Pointi A upandeni mwa kiganja na kusema:

"Ingawa nina tatizo hili,. . Niko salama, Najikubali nafsi yangu."

4. Rudia hatua ya 2 na ya 3

Rudia mfuatano mpaka kiwango cha wasiwasi kimefikia 0 - 2.

5. Fikicha Pointi B inayouma:

Fikicha pointi inayouma upande wa kushoto

kama inchi 3 chini ya mtulinga na inchi 2 - 3 upande wa kidari.

KUSHIKA SEHEMU ZA MWILI

Zoezi hili ni la namna rahisi ya kushika sehemu za mwili ambalo unaweza kujifanyia mwenyewe au kumfanyia

mwingine kwa ajili ya kuondoa wasiwasi, maumivu ya mwilini na machungu na majeraha ya moyoni. Pia kumbukumbu

kali za athari za majanga, hisia kali kama vile hasira au hofu, kukosa usingizi na kwa mburudiko wa kina. Kupitia nguvu

katika mikono yetu, tunao uwezo wa kuleta amani ya kina, upatanisho/ulinganifu na uponaji wa mwili, akili na

mhemuko. Unapojifanyia au kumfanyia mwingine zoezi hili, fikiria akilini na moyoni amani ya kina, wepesi na nafasi.

Unaweza kushika kwa dakika chache kila sehemu huku ukipumua kwa kina tumboni ili kukuza kuachia. Shika kwa

ulaini kabisa, kama mtu anaogopa kuguswa kwa sababu ya maumivu au historia ya kutumiwa vibaya, fanya zoezi juu

ya mwili wake katika eneo lake la nguvu. Wakati wote omba ruhusa kabla ya kumgusa mwingine kwenye zoezi lolote.

Kushika Halo

Kushika Kichwa:

Mkono mmoja unashikapaji la uso, mwingineunashika kisogo. Nguvu ya mikono

inaungana na sehemu za ubongo zinazohusiana na Kumbukumbu.

Kushika Utosi:

Vidole gumba vyote viwili vinagusa utosi. Vidole vingine vinagusa kwenye paji la uso

Pamoja na kupumua kwa kina, zoezi hili Hutumiwa mazoezi mbalimbali ya mwili ili kutoa

nguvu iliyoziba.

Kushika Mabega:

Viganja vinagusa mabega, mahali Mwilini ambapo panahusika wasiwasi, mizigo ya

ziada au masumbufu ya maisha.

Kushika Moyo:

Mkono mmoja unashika katikati ya Kifua. Mkono mwingine unagusa Mgongoni nyuma

ya moyo. Eneo la moyo mara nyingi hubeba maumivu ya hisia, majeraha ya zamani,

majonzi na maudhi. Pumua kwa kina na ufikiri kuwa maumivu ya moyo yanatiririka na

kutoka hadi ardhini.

Kwa kumaliza: Taratibu pangusa eneo lake la nguvu kwa mikono yako. Pia unaweza kufunika miguu yake kwa viganja vyako ili kumsimika

KICHWA, SHINGO, MABEGA KUACHWA HURU

Zoezi hili la acupressure ni lenye nguvu katika kuondoa msongo na maumivu kwenye mgongo, mabega, shingo na kichwa. Mara nyingi kutokana

na athari za majanga (trauma) na msongo wa mambo (stress), nguvu huziba kwenye mabega, shingo na kichwa na hii hujitokeza kama maumivu,

mfadhaiko na msongamano. Meridiani au mifereji ya nguvu iliyo mingi hutiririka kwenye eneo hili na kusababisha “shingo ya chupa” ya mfadhaiko

kwa baadhi ya watu. Zoezi hili huweza mtu kujifanyia au kumfanyia mtu mwingine akiwa amekaa au amelala vizuri chali. Kama unafanya na mtu

mwingine, hakikisha unaweka mipaka wazi na ikiwa ukisikia nguvu yake inaingia kwenye mikono yako, fikiria kuwa inaweza kutiririka na kupita hadi

ardhini. Kwa vidole vilivyokunjwa kidogo, bonyeza kwenye kila seti ya pointi 1-6 kwa dakika 1 hadi 2, au mpaka mapigo ya nguvu yawe wazi, imara

na yanatiririka. Pointi hizi kwa kawaida zinauma.Wakati wa zoezi unaweza kufikiria nguvu ikitiririka kwenda juu na kutokea kichwani huku ukiwa

unapumua kwa kina. Kwa kumalizia zoezi, fikiria kuwa miguu yako imeota ardhini kukusimika. Kama unamfanyia mtu mwingine unaweza kushika

miguu yake kwa dakika chache ili kumsimika.

( Limetolewa kutoka kazi ya Aminah Raheem na lona Teegarden).

Kwa kumaliza:

Shika miguuni kwa kumsimika. Ukijifanyia mwenyewe, fikiria

kuwa miguu imesimikwa ardhini. Pumua kwa kina na usikie

amani na ulinganifu katika mwili, akili, roho.

‘ACUPRESSURE’ KWA MAUMIVU NA ATHARI ZA MSONGO

Mfadhaiko:

Pointi hizi za ‘acupressure’ ni kwa ajili ya mfadhaiko na uzito wa hisia kali ili kuleta amani na uzima.

Utosini:

Shika utosini taratibu. Kuna pointi tatu sehemu hii zinazofuatana katika msitari.

Paji la Uso katikati ya Nyusi:

Kwa ncha za vidole vya mkono mmoja, shika sehemu ya katikati ya nyusi mahali ambapo pua huungana na paji la uso.

Chini ya Kisogo kila upande wa kichwa:

Pishanisha vidole na uweke mikono nyuma ya kichwa, vidole gumba vikikandamiza kushoto na kulia chini ya kisogo katikati ya

misuri na mifupa.

Wasiwasi na Hali ya Hatari:

Pointi nje ya kifundo cha mkono, kandamiza pointi inayoingia nje ya mkunjo wa kifundo cha mkono chini ya kidole kidogo.

Pointi Juu ya Mabega:

Kwa ncha za vidole vya mikono yote miwili shika pointi juu ya mabega. Mikono inaweza kupishana

kama hali hii ni nzuri zaidi.

Sehemu inayouma:

Tafuta sehemu inayouma upande wa kushoto wa kifua kama inchi 2 – 3 chini ya mtulinga na kama

inchi 2 upande wa mfupa wa kidari.

Kuzimia, Hali ya Hatari na Shinikizo la Damu:

Pointi hii inaweza kutumiwa na wewe mwenyewe au mtu mwingine anayezimia

au yuko kwenye hali ya hatari.

Pointi chini ya Pua:

Kwa kidole cha Shahada au Konzi ya kidole, kandamiza kwenye pointi chini ya

pua mdomo wa juu.

Kukosa Usingizi:

Pointi kwenye Paji la Uso na Pointi katikati ya kifua.

Shika kwa wakati mmoja pointi iliyo katikati ya paji la uso na pointi iliyo katikati ya kifua.




Jumamosi, Juni 04, 2011

UFUNUO WA MWISHO

Waebr. 1:1-3.

Azimio: Ufunuo mkamilifu na wa mwisho wa Mungu unapatikana ndani ya Kristo na

katika mafundisho Yake.

Shabaha: Kuonyesha kwamba Yesu Kristo na Agano Jipya ni ufunuo wa mwisho wa

Mungu kwa mwanadamu.

Dibaji: Jifikirie kuwa u Myahudi aliyeishi kama miaka 1880 iliyopita, ikiwa ni mle

Yerusalemu au Palestina, chini ya kongwa 1a ugandamizaji wa Warumi. Tabia ya

kuipenda nchi yao inaanza kuwaka miongoni mwa ndugu wa Kiyahudi wanaofanya

mipango ya kuasi. Kuna lalamiko la utukufu uliopita (historia yao), kuna lalamiko na

kupendeza kwa ibada yao ya kale (sheria ya Musa), wanalo hekalu kubwa, ukuhani wa

ajabu na sadaka za kuongoza mawazo yao na kuwageuza kutoka kwa Kristo. Yote haya



Mataifa hawakuwa katika hatari iliyo tofauti ya kurudia miungu yao; wengine wao bila

shaka walirudia katika tabia na mazoezi yao ya zamani, lakini sio katika miungu ya

washenzi; kwa Wayahudi ilikuwa tofauti, kwani Yehova alikuwa ni Mungu wa wakale na

wapya pia.

Waraka huu kwa Waebrania ulikuwa wa kuonyesha kuwa la zamani limerithiwa na jipya,

utukufu wa jipya ni mkuu kuliko utukufu wa la kale. Kwa hiyo, ombi la kuwa imara

linafanywa katika msingi huu. Neno la ufunguo ni "bora" kusihi katika waraka mzima ni

"kuwa imara."

----------------------------------------------------------

Ndugu msomaji: MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Walter L. Pearson Jr.

Anapotwambia:



Ijumaa, Juni 03, 2011

Bunilizi ya kinjozi





Bunilizi ya kinjozi (au bunilizi ya kifantasia) ni utanzu fulani wa fasihi andishi. Katika bunilizi hiyo mwandishi anatumia matukio au wahusika wasio wa kawaida.

Mifano ya bunilizi ya kinjozi katika fasihi ya Kiingereza ni "A Midsummer Night's Dream" (Ndoto ya Usiku Mmoja) ya William Shakespeare, "Gulliver's Travels" (Safari za Guliveri) ya Jonathan Swift, au "The Lord of the Rings" (Bwana wa Mapete) ya J.R.R. Tolkien.

Bunilizi ya kinjozi hutofautishwa na bunilizi ya kisayansi kwa vile haisifu mambo ya teknolojia bali inatumia maajabu na viumbe vya visasili.