Ndugu mpendwa, ni vyema sana kuwa nawe tena katika eneo hili.
Tuko
hapa duniani katika kipindi cha ajabu katika historia yake. Nafasi zetu
karibu hazina kipimo, na bado tunakumbana pia na changamoto nyingi,
baadhi yazo za kipekee kwa wakati wetu.
Tunaishi
katika ulimwengu ambapo maadili yametupiliwa mbali kwa kiasi kikubwa,
ambapo dhambi imeanikwa wazi, na ambapo majaribu kupotoka kutoka kwenye
njia nyembamba na iliyosonga yanatuzunguka. Tunakabiliwa na mashinikizo
yasiyokoma na ushawishi wa kudanganya unaoharibu kile ambacho ni cha
heshima na kujaribu kukibadilisha na falsafa na utamaduni duni.
Kwa
sababu hizi na changamoto zingine, maamuzi daima yako mbele yetu ambayo
yanaweza kuamua hatima yetu. Ili kwetu sisi kufanya maamuzi sahihi,
ujasiri unahitajika---ujasiri wa kusema hapana wakati tunapaswa, ujasiri
wa kusema ndio wakati inafaa, ujasiri wa kufanya jambo la haki kwa
sababu ni la haki.
Kwa
sababu viwango vya jamii hivi sasa kwa haraka vinaachana kwa mbali na
maadili na kanuni ambazo Bwana ametupa, sisi bila shaka tutaitwa kutetea
kile ambacho tunaamini. Je, tutakuwa na ujasiri wa kufanya hivyo?
Rais
J. Reuben Clark Jr., ambaye kwa miaka mingi alikuwa mshiriki wa Urais
wa Kwanza, alisema: “Zinajulikana kesi ambapo [wale] wa imani ya
kudhaniwa … wamehisi kwamba, kwa sababu ya kudhibitisha imani yao kamili
huenda wakajiitia kejeli ya wenzao wasioamini, lazima aidha warekebishe
au kuelezea vyema imani yao, ama kuizimua kiuangamizi, ama hata
kujifanya kuitupilia mbali. Watu kama hao ni wanafiki.” Hakuna yeyote miongoni mwetu angependa kuitwa mnafiki, na bado tunasita kutangaza imani yetu katika hali fulani. ?
Tunaweza
kujisaidia katika hamu yetu ya kufanya mema tukijiweka katika maeneo na
kushiriki katika shughuli ambapo mawazo yetu yanashawishiwa kwa ajili
ya mema na ambapo Roho wa Bwana atasikia vizuri kuwa.
Nakumbuka
nikisoma hapo awali ushauri ambao baba alimpa mwanawe wakati akienda
shule: “Ukiwahi kujipata mahali ambapo haupaswi kuwa, ondoka!” Nawapa
kila mmoja wenu ushauri huo huo: “Ukijikuta wakati wowote mahali ambapo
haupaswi kuwa, ondoka!”
Sote
tunahitaji kila mara kuwa na ujasiri. Kila siku ya maisha yetu ujasiri
unahitajika---si tu kwa ajili ya matukio makubwa, lakini mara nyingi
zaidi tunapofanya maamuzi ama kutenda kwa ajili ya hali zilizo karibu
nasi. Mshairi na mwandishi Mskoti Robert Louis Stevenson alisema: “Kila
siku ujasiri una mashahidi wachache. Lakini ujasiri wako bado una
heshima hata kama hakuna anayekutia moyo na hakuna umati unaokusifu.”
Ujasiri
huja kwa njia nyingi. Mwandishi Mkristo Charles Swindoll aliandika:
“Ujasiri hauko tu kwenye uwanja wa vita … ama kwa kumshika kiushujaa
mwizi katika nyumba yako. Vipimo halisi vya ujasiri ni kimya sana. Ni
majaribio ya kindani, kama vile kubaki mwaminifu wakati hakuna mtu
anayeangalia, … kama kusimama peke yako wakati watu hawaelewi imani
yako.”
Ningeongezea kwamba ujasiri huu wa ndani pia unajumuisha kufanya jambo
la haki hata kama huenda kuwa unahofia, kutetea imani yetu katika hatari
ya kudharauliwa , na kudumisha imani hizo hata baada ya kutishwa na
kupoteza marafiki ama hadhi ya kijamii. Yule ambaye anasimama dhabiti
kwa yale ambayo ni ya haki lazima ahatarishe kuwa wakati mwingine
hakubaliwi na kukosa umaarufu.
Mtu mmoja alipokuwa akihudumu katika Jeshi la Majini la Marekani alikuja kujua kuhusu
matendo ya ujasiri, matukio ya ushujaa, na mifano ya ujasiri. Mmoja
ambao kamwe hakuwahi sahau ilikuwa ujasiri usio wazi wa mwana maji wa
umri wa miaka 18---sio wa imani yetu---ambaye hakuogopa kusali.
Kwa watu
250 katika kitengo chetu, alikuwa ndiye peke yake ambaye kila usiku
alipiga magoti kando ya kitanda chake, wakati mwingine akiwa anakejeliwa
na kuchekwa na wasioamini. Akiwa ameinamisha kichwa, alimwomba Mungu.
Kamwe hakuogopa kuomba. Kamwe hakuyumba. Alikuwa na ujasiri.
Muda
mfupi uliopita, nilisikiliza mfano wa mtu ambaye hakika alionekana
kukosa ujasiri huu wa ndani. Rafiki alisimulia kuhusu mkutano wa kiroho na wa kukuza imani ambao yeye na mumewe walikuwa
wamehudhuria katika kata yao.
Mvulana aliyekuwa katika ofisi ya mkuhani
katika Ukuhani wa Haruni aligusa mioyo ya mkusanyiko mzima
alipozungumzia kweli za injili na furaha za kutii amri. Alishuhudia kwa
dhati akisimama kwenye mimbari, akionekana kuwa msafi na nadhifu akiwa
amevaa shati yake nyeupe na tai.
Baadaye
siku hiyo hiyo, mwanamke huyu na mumewe walipokuwa wanaondoka kule,
walimuona mvulana yule yule ambaye alikuwa amewavutia sana saa chache tu
awali. Sasa, hata hivyo, alionekana kubadilika kabisa akitembea
barabarani akiwa amevaa nguo chafu---na anavuta sigara.
Rafiki yangu na
mumewe hawakuwa wamesikitishwa sana na kuhuzunika tu, lakini pia
walichanganyikiwa na jinsi angeweza kusadikisha kuonekana kuwa mtu mmoja
katika mkutano wa kiroho na kisha haraka hivyo kuonekana kuwa mtu
mwingine kabisa.
Ndugu,
je, wewe ni mtu yule yule popote ulipo na katika chochote
unachofanya---mtu Baba yetu wa Mbinguni anataka uwe na mtu unajua
unapaswa kuwa?
Katika
mahojiano yaliyochapishwa katika gazeti la kitaifa, mchezaji
aliyejulikana wa mpira wa kikapu wa NCAA Mmarekani anayeitwa Jabari
Parker, mshiriki wa Kanisa, aliombwa ashiriki ushauri bora kabisa
aliokuwa amepokea kutoka kwa baba yake. Jabari alijibu, “[Baba Yangu]
alisema, kuwa mtu yule yule unapokuwa peke yako na vivyo hivyo unapokuwa
mbele ya watu.” Ushauri muhimu, ndugu zangu, kwetu sisi sote.
Maandiko
yetu yamejaa mifano ya aina ya ujasiri unaohitajika na kila mmoja wetu
leo. Nabii Danieli alionyesha ujasiri mkuu kutetea aliyoyajua kuwa ya
haki na kwa kuonyesha ujasiri wa kuomba, ingawa alitishwa na kifo kama
angefanya hivyo.
Abinadi aliishi maisha ya ujasiri, ilivyoonyeshwa na kukubali kifo badala ya kukana ukweli.
Sisi
sote tunavutiwa na maisha ya vijana askari 2,000 wana wa Helamani,
waliofundisha na kuonyesha umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kufuata
mafundisho ya wazazi, kuwa waadilifu na wasafi?
Pengine
kila moja ya hadithi hizi za maandiko zimepambwa na mfano wa Moroni,
ambaye alikuwa na ujasiri wa kustahimili katika haki hadi mwisho
Katika
maisha yake yote, Nabii Joseph Smith alitoa mifano isiyohesabika ya
ujasiri. Mojawapo wa mfano mkubwa zaidi ulitokea wakati yeye na ndugu
wengine walifungwa minyororo pamoja---fikiria, kufungwa minyororo
pamoja---na kufungiwa katika nyumba ambayo haijamalizika karibu na jumba
la mahakama kule Richmond, Missouri. Parley P. Pratt, ambaye alikuwa
miongoni mwa wale waliofungwa, aliandika kuhusu usiku mmoja:
“Tulikuwa
tumelala ni kama tuko usingizini mpaka saa ya usiku wa manane kupita, na
tulikuwa tumehuzunika sana, wakati tulikuwa tumesikiliza kwa masaa
kejeli mbaya, maneno mabaya, kashfa kubwa na lugha chafu ya walinzi
wetu.”
Mzee Pratt aliendelea:
“Nilikuwa
nimesikiliza hadi nikachukizwa, nikasikitika, nikahudhika , na kujawa
na roho ya haki ya kukasirika kwamba ilikuwa vigumu kwangu kujizuia
kusimama na kuwakemea walinzi, lakini [mimi] sikuwa nimemwambia Joseph
chochote, ama mtu yeyote mwingine, ingawa nilikuwa nimelala karibu naye
na nilijua kwamba alikuwa macho. Ghafla, alisimama na kuzungumza kwa
sauti ya nguvu kama mgurumo wa simba, akisema, vyema ninavyoweza
kukumbuka, maneno yafuatayo:
“‘NYAMAZENI.
... Katika jina la Yesu Kristo nawakemea ninyi, na kuwaamurisha mtulie;
sitaishi dakika ingine na kusikia lugha kama hiyo. Komeni kuongea
hivyo, ama ninyi au mimi nife SAA HII!’”
Joseph
“alisimama wima katika enzi ya kutisha,” kama ilivyoelezwa na Mzee
Pratt. Alikuwa amefungwa kwa minyororo, bila silaha, na bado alikuwa
mtulivu na mwenye heshima. Aliwaangalia walinzi waliohofia, ambao
walikuwa wanarudi nyuma kwenye kona wakijikunyata miguu. Watu hawa
walioonekana kutorekebishika waliomba msamaha kwake na wakabaki kimya.
Si
vitendo vyote vya ujasiri huleta matokeo ya kuvutia kama hayo ama ya
mara moja, na bado yote huleta amani akilini na maarifa kwamba haki na
ukweli umetetewa.
Ni
vigumu kusimama wima wakati mtu anapanda mizizi yake kwenye changarawe
inayonyong’onyea ya maoni na idhinisho linalobobea. Ujasiri kama ule wa
Danieli, Abinadi, Moroni ama Joseph Smith unahitajika ili tubaki imara
na dhabiti kwa yale tunayojua ni mema. Walikuwa na ujasiri wa kufanya
kile ambacho akikuwa rahisi, bali kile kilichokuwa sahihi.
Sote
tutakumbana na hofu, tutakejeliliwa, na kukutana na upinzani. Acheni
sisi —sisi sote—tuwe na ujasiri kushinda yanayopendelewa na wengi,
ujasiri wa kutetea kanuni zetu. Ujasiri, si kuridhisha, hutuletea
tabasamu ya idhini ya Mungu. Ujasiri unakuwa sifa ya uwezo na ya kuvutia
wakati unachukuliwa si tu kama nia ya kufa kidume lakini pia kama
uamuzi wa kuishi kwa heshima.
Tunavyosonga mbele, tukijitahidi kuishi
kama tunavyopaswa, hakika tutapokea msaada kutoka kwa Bwana na tunaweza
kupata faraja katika maneno Yake. Naipenda ahadi Yake katika kitabu cha
Yoshua: “Sitakupungukia wala sitakuacha. …
“...Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”
Ndugu yangu mpendwa, kwa ujasiri wa imani yetu, tutangazeni, pamoja na Mtume Paulo, “Siionei haya Injili ya Kristo.”Kisha,
kwa ujasiri huo huo, tufuateni ushauri wa Paulo : “Uwe kielelezo kwao
waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo, na katika roho na
imani na usafi.”
Migogoro
ya janga huja na kwenda, lakini vita vinavyopigwa kwa nafsi za watu
vinaendelea bila kukoma. Kama mwito linakuja neno la Bwana kwenu, kwangu
mimi, na kwa wenye ukuhani kila mahali:
“Kwa sababu hiyo, sasa acha
kila mtu na ajifunze wajibu wake, na kutenda kazi katika ofisi ambayo
ameteuliwa, kwa bidii yote.” Kisha tutakuwa, kama vile Mtume Petro alivyotangaza, hata “ukuhani wa kifalme,”na umoja katika kusudi na kubarikiwa na nguvu kutoka mbinguni.
Acha
kila mmoja wetu aondoke siku ya leo akiwa na dhamira na ujasiri wa
kusema, pamoja na Ayubu wa kale, “Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani
yangu,...sitajiondolea uelekevu wangu.”
Naomba kwa unyenyekevu kwamba hii iweze kuwa hivyo katika jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Amina.