Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Oktoba 15, 2013

SEKTA ZA UCHUMIUchumi wa kijadi katika nchi nyingi ulikuwa hasa kilimo cha kujikimu pamoja na biashara ya kubadilishana bishaa kadhaa zenye thamani kubwa. Kwa mfano tangu kale migodi ya Zimbabwe ilichimba dhahabu iliyopelekwa baadaye hadi Asia na dunia ya Mediteranea.
Katika uchumi wa kisasa mara nyinga sekta tatu hutofautishwa:
  • Sekta ya msingi: kutoa na kuzaa malighafi pamoja na mazao katika mazingira asilia. Mifano ni kilimo, uchimbaji wa madini, uvuvi au kuvuna ubao.
  • Sekta ya pili: shughuli za kubadilisha malighafi hizi kuwa bidhaa. Madini ya chuma hubadilishwa kuwa feleji; feleji hutumiwa na viwanda kutengeneza vyuma vya ujenzi, magari, vifaa vya nyumbani. Viwanda vya nguo hutumia pamba kutoka mashambani na kuibadilisha kuwa uzi halafu kitambaa na nguo.
  • Sekta ya tatu: biashara au usambazaji wa bidhaa hizi kwa wateja pamoja na kuwatolea huduma. Mifano ni maduka yanayouza bidhaa zilizotengenezwa viwandani. Mingine ni huduma kama benki, hoteli, sinema na usafiri.
  • Wataalamu wengine hutaja sekta ya nne: shughuli za kusambaza habari na pia utafiti wa teknolojia mpya unaoendelea kuwa muhimu katika nchi zinazoendelea. Wengine huingiza pia elimu (kazi za shule na vyuo) katika sekta hiiy a uchumi.

Sayansi ya Uchumi

Hii ni mkono wa elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.  


Uchumi ni jumla ya shughuli zote za kibinadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji ya watu. Ni hasa shughuli za uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.
Uchumi mara nyingi hutazamiwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni