Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Desemba 22, 2011

MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM


Jiji la Dar es salaam limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha, unaweza dhani nisimulizi ila kihalisia wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake ndio wanajua uzito wa hali inayowakabili wakazi wengi.

Jiji la Dar es salaam linachangamoto ya foleni hasa kwa upande wa magari. Picha chini ni namna maji yalivyoiharibu barabara na kisha kusababisha gari kutumbukia katika mtaro wakati likiwa katika foleni. HEBU FIKIRIA KAMA MMILIKI WA GARI ALILIPATA KWA NJIA YA MKOPO!!



Hata magari ya zimamoto yalikumbwa na adha hiyo na ukiangalia hakuna njia ya haraka ya kuweza kusaidia kuokoa gari kama hili lililokutwa na maji wakati likiwa katika foleni (msongamano). Na yumkini kuna mahali lilikuwa linaelekea kuaokoa watu.





Taarifa zilizopatikana ni kwamba wanajeshi wanajaribu kuokoa wana nchi katika baadhi ya maeneo,


Picha hizi ni za maeneo mbalimbali na zimepigwa na wadau walioguswa na tukio hili la kusikitisha.
Mafuriko yazusha shida kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam, naamini utakuwa umejionea ama kusikia habari mbalimbali kupitia Televisheni, Radio, Magazeti, Mitandao. Hali ndivyo ilivyo na bado mvua zinaonesha hali yakuendelea kunyesha.






Na usishangae serikali ikaunda tume ya kuchunguza mafuriko!!!


MAOMBI NA MSAADA WAKO NI WA MUHIMU KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALIOKUMBWA NA ADHA HII YA MAFURIKO. JIHOJI MWENYE KAMA YANGEKUKUTA WEWE UNGEFANYAJE!?







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni