Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Januari 14, 2011

VICHEKESHO (FUTUHI) COMEDY

Wachekeshaji (comedians) ni wasanii ambao wana umuhimu wa aina yake katika jam

Hawa ndio hufanya wakati mwingi watu tusahau uchungu wa maisha kwa jinsi ambavyo wanatuvunja mbavu tukiwasikiliza radioni, kuwaona kwenye luninga au hata kukutana nao mitaani. Si unakumbuka tangu enzi za akina Mahoka…enzi za akina Pwagu na Pwaguzi?

Kwa bahati mbaya sana nchini Tanzania bado hakuna mifumo mizuri kwa ajili ya wasanii kama hawa kufaidi vizuri jasho lao. Wengi wao wanakuwa na hali za kimaisha ambazo hazilingani na vipaji walivyonavyo. Isitoshe wasanii hawa, kwa kupitia michezo au vichekesho vyao hutoa mafunzo mazuri sana ya ya kijamii na katika jamii. Tatizo huwa linakuwa wapi katika kutengeneza mifumo imara ambayo itahakikisha wasanii wanafaidika? Swali hili linaelekea kuzidi kuwa gumu japo sasa mwanga unaonekana siku hadi siku.

Hatupendi kulirudia rudia lakini tunathamini sana mchango wako msomaji wangu katika kubadilishana mambo kadhaa ambayo kwa hakika yanawezekana kabisa.

Maoni 1 :

  1. jamani mbona wanamwaga radhi hahaha hayo matunda hatununui ng`o.

    JibuFuta