Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Januari 26, 2011

MORNING STAR RADIO 105.3 FM-DSM

Njozi za kuanzishwa kwa Radio hii, ilianzia katika miaka ya tisini, ambapo mwaka 2000 viongozi wa makanisa ya Dar es salaam walikutana na kuweka mkakati madhubuti wa kuanzisha radio hii kwa wakati huo ikijulikana kama TAWR (Tanzania Adventist World Radio).

Mwaka 2001, uchunguzi yakinifu wa kuanzishwa kwa Kituo hiki ulianza chini ya kitengo cha mawasiliano cha Makao makuu ya Kanisa Tanzania kijulikanacho kama TAMC (Tanzania Adventist Media Center).

Baada ya mikakati madhubuti kukamilika, ujenzi wa kituo cha radio ulianza rasmi mnamo mwaka 2002, katika eneo la Mikocheni B, jijini Dar es salaam, ujenzi ambao uliendelea na kukamilika kwa sehemu kubwa mnamo mwaka 2003.

Mnamo tarehe moja mwezi wa kumi mwaka 2003, kituo kilirusha matangazo yake kwa mara ya kwanza kama majaribio, kwa kutumia mtambo wa kurushia matangazo wenye uwezo wa watt 500, na tangu hapo safari ya matangazo kusikika hewani iliendelea!

Mwezi wa kumi na moja mwaka wa 2003, kituo kilifunguliwa rasmi na Mgeni aliyehudhuria
shughuli hiyo, Mchungaji Jan Paulsen, akija kama Rais wa kanisa la Waadventista wasabato Duniani, akitoea Nchini Marekani ambako ndiko makao makuu ya Kanisa Duniani, yalipo.

Majuma mawili baada ya kufunguliwa rasmi kwa kituo, Mtambo wa kurushia matangazo
uliokuwa umefungwa mikocheni B mahali zilipo studio, ulishindwa kufanya kazi kutokana na hitilafu iliyosababishwa na umeme, tatizo lililojitokeza baada ya mvua kali kunyesha.

Jitihada za kujaribu kuirejesha katika hali ya kuendelea kufanya kazi zilishindikana, jambo lililopelekea muingiliano na vyombo vingine vya habari, na kituo kufungwa kwa muda na tume ya mawasilianona, ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa marekebisho. Kituo kilirejea tena katika hali yake na kuendelea na matangazo baada ya miaka miwili baadae.

Mwaka 2005 mwezi wa tano,vifaa vipya vya kurushia matangazo viliagizwa ili kurejesha matangazo tena. Uagizaji huo ulichukua muda wa miezi mitatu, na mwezi wa nane vifaa viliwasili na ufungaji ukaanza mara moja, wakati huu mtambo ukiwa umehamishiwa eneo la kisarawe, mkoa wa Pwani.

Baada ya ufungaji mtambo kukamilika, mnamo mwezi wa nane mwaka 2005, urushaji wa matangazo ya majaribio ulianza mara moja, ambapo majaribio hayo yalichukua takribani mwezi mmoja, hadi mnamo mwezi wa tisa!

Ilipofika tarehe 26, mwezi wa tano mwaka 2006, saa 11:00 jioni, kituo kilirusha matangazo moja kwa moja kwa mara ya kwanza, baada ya matangazo ya majaribio
kukamilika!

Tangu hapo, Morning Star Radio imeendelea kurusha matangazo yake hadi hivi sasa, ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakibarikiwa sana na matangazo haya, na kwa hakika kituo hiki kimekuwa ni mbaraka sana kwa ma elfu ya wakaazi wa Tanzania na dunia kwa ujumla ambapo matangazo ya Redio hii yanasikika!


Morning Star Radio inakuletea habari za dunia katika eneo lote la Afrika Mashariki na kati pamoja na kanda ya Maziwa Makuu kwa lugha ya Kiswahili kutoka Dar es Salaam, Tanzania, chimbuko la lugha adhimu ya Kiswahili inayokua kwa kasi.

Idhaa ya Kiswahili ya Morning Star Radio inakuletea habari, makala na uchambuzi pia taarifa za burudani kwa lugha ya Kiswahili kwa wasikilizaji wa Afrika ya Mashariki na kati pamoja na kanda ya Maziwa Makuu kupitia mtandao wa vituo 17 vilivyo jiunga na Morning Star Radio kwa Masafa ya FM kupitia satelite.

Sikiliza matangazo ya Morning Star Radio kila siku kwa muda wa masaa 24 saa za afrika mashariki
.

Tutakuwa tunawafikia watu milioni 100 hadi milioni 150 wanaotumia lugha ya Kiswahili kila siku. Morning Star Radio kwa sasa inarusha hewani matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili na kwa uchache sana pia lugha ya kiingereza kwa njia ya Satellite kupitia Hope Channel International.

Maoni 6 :

  1. Ahsante kaka Mcharia,baraka na maendeleo mema!

    JibuFuta
  2. habari za leo!!
    inawezekana hii si njia nzuri sana ya kuwasiliana na radio lakini naona kama nimeshindwa kuwasiliana na uongozi wa morning star. naomba email ya uongozi au simu ningependa kuwasilisha habari muhimu zenye msaada kwa radio.
    mbasamnyau@yahoo.com

    JibuFuta
  3. Hii redio inabariki sana,kwanza vipindi vyake vinaelimisha Mungu aendelee kuwapa nguvu pia akili wafanyakazi hususani watayarishaji wa vipindi.Ingawa huku kwetu Korogwe kuna muda inakuwa inasikika kwa taabu sana.

    JibuFuta