Sababu kubwa ya tatizo hili ni:
1.Kuvaa nguo ya ndani kwa muda mrefu...
2.Kuvaa nguo ya ndani bila ya kujikausha vizuri hivyo kubakiwa na unyevu..
3. Kuvaa nguo za ndani zisizoendana na khali ya hewa ya eneo uloishi...
4. kushindwa kuoga au kujisafisha nyeti baada ya kumaliza kuzini au kufanya tendo la ndoa kwa walio oa!

Jitahidi kuoga mara tatu kwa siku au mbili kama ni mtu uliye bize na kazi...na mara baada ya kuoga jikaushe vizuri kwa kutumia taulo lililotengenezwa kwa pamba.
Boxers au chupi za material ya mpira si nzuri kwa mikoa ya joto kama Dar es salaam, Morogoro na dodoma kwa kuwa zinasababisha joto amablo hupelekea kutoa harufu....
Vaa boxer za matelia ya pamba ni bora zaidi na kufanya maeneo nyeti kuwa makavu wakati wote.

Nakuhakikishia ukifanya hivyo uatakuwa msafi na kuvutia muda wote hata mahusiano yako na mpenzi wako yatadumu na kuwa yafuraha zaidi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni