Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Novemba 11, 2010

MEZA YA MAOMBI KILA J5 NA J'PILI

HAYA NI MAHITAJI YA KUOMBEA YALIYOTUFIKIA KATIKA KIPINDI CHA
ANZA NA BWANA AMBACHO KILIRUSHWA 105.3 FM
SIKU YA Jumatano 10th, November, 2010
KATIKA WASAA WA MEZA YA MAOMBI.
JAMBO HILI HUFANYIKA KILA JUMAPILI NA JUMATANO
KUANZIA SAA
11:00 ALFAJIRI - 12:00 ASUBUHI.

1. Bwana Apewe Sifa Ndugu Yusufu.Nasema Ahsante kwa Maombi yenu.Naomba Mniombee maana leo naenda kufanya Interview saa mbili ili niweze kufaulu na kupata kazi.Ahsante na Mbarikiwe sana!.

2. Bwana apewe sifa!,Naomba mniombee Mungu aniponye kwani huu ni mwezi wa pili naumwa- nipo Banana!.

3. BWANA APEWE SIFA. NAOMBA MUNGU KWA KUTUAMSHA SALAMA SIKU YA LEO PIA ATUBARIKI SIKU ZOTE ZA MAISHA YETU NA WENYE SHIDA WENYE HUZUNI MUNGU AWAPE NGUVU

4. Bwana asifiwe ,naomba mniombe kazi za mikono yangu ziwe za mafanikio.

5. Bwana asifiwe naomba mniombee mapenzi yatimie katika ndoa yetu itakayofungwa mwenzi wa kumi na mbili naomba tuliweke miguuni pa yesu

6. Bwana asifiwe sana,naamini Bwana akipenda kaka yangu Abeid mifupa yake itaimarishwa na hatahitaji kufanyiwa operation, yuko MOI.Mbarikiwe hapo studio kwa somo zuri, nipo Ilala.

7. Bwana asifiwe, naenda kufanya enterview naomba mniombee Yesu aniongoze na niipate hii kazi kama ni mpango wa Bwana.

8. BWANA ASIFIWE. NAOMBA MUNGU ANIBARI KTK KAZI YANGU ANIEPUSHE NA MAPITO MAGUMU NIWEZESHE KTK MAISHA YANGU. NIKO CHAMAZI KWA MKONGO .

9. Bwana asifiwe.mm ni mama mjane naomba mniombe na familia yangu watoto wangu waxe vichwa na si mikia katka masomo yao. NIPO TABATA.¬

10. Bwana Yesu apewe sifa..!naomba mniombee macho yananisumbua sana,asante mbarkiwe, nipo ubungo.


11. Bwana Yesu asifiwe,naomba mumuombee dada yangu aache madawa ya kulevya na kaka yangt aache pombe.pia namshukuru Mungu kwa kuwa amenitendea miujiza na naomba mniombee kampuni ninayofungua ikamilike na pia biashara ninayoanza leo iwe ni mbaraka katika maisha yangu.Mungu awabariki hapo studio.

12. BWANA YESU ASIFIWE. NAOMBA MAOMBI KWAAJILI YA MUMEWANGU ANASUMBULIWA NA MOYO UMETANUKA. NIPO BANANA.

13. Elieza Asraji: kulinga na lmaniyangu ya usabato napitia changamoto nyingi.mniombee MUNGU anipe imani imara. Muombeeni babangu arudisheupendo,kwangu mimi mwanawe,ingawaje nimezaliwanjeyandoa,pia yeye mwisram,mimi msabato na usabato wangu wanidharau kweli. Tuombee koo hizi,ukoowa Asraji,sala,joji,mpole,mama Asha Sef,j.Bada.koohizi zimepungukiwa ROHO MTAKATIFU.mungu aingiliekati kiroho na kimwili.

14. Habar y asubuhi hapo studio mungu awa bariki cn na mahur mazur naomba mumuombe bi b naumwa kichwa na mm pia uniombe niwe na afya nzur il niweze kufanya vizur shulen.

15. Habari za asubuhi studio.nahitaji mniombee nipate school fees kwa ajili ya chuo.pia muiombee familia yangu.

16. Halo Mr. Yusufu hapo Morning star mna nyimbo nzuri ambazo hazipatikani kwenye maduka ya nyimbo. Je hapo morning star mnauza CD/kanda za nyimbo? Nipo magomen

17. M/STAR MBARIKIWE.BABA YANGU ANAOMBA AOMBEWE MAOMBIYA TOBA REUBEN NEHEMIA NA MJUKUU WAKE WA JINA LAKE AACHE POMBE .

18. mbariki we naomba mniombe mimi fundi ujenzi nipateka kazi

19. Mbarikiwe hapo studio,ninawaomba mniombee kwa ajili ya kampuni zangu ambazo zipo kwenye interview,natanguliza shukrani zangu kwa Bwana.


20. MBARIKIWE WATUMISHI NAOMBA MAOMBI KWA AJILI YA BIASHARA NIPATE KUUZA NI WAWA MNDEWA

21. Mbarikiwe watumishi wa Mungu mniombee haya yafuatayo mama yangu apone apate kumbukumbu ya ufahamu na mwanangu aendelee kutulia arudie tabia yake ya utulivu

22. Mimi ni mshiriki mwadventista nina umri wa miaka 10 kanisani nina miaka 33 sina mume na nimemuomba mungu miaka 10 yote na mungu amenyamaza na ninamwomba sana mungu aniepushe na jarabu la uzinzi lakini imefika sehemu nimeanguka ktk jaribu la uzinzi na moyo wangu umekosa amani kwa mungu wangu nisaidieni ijapo niko ije ya maada nielewesheni na muniombee niishinde hiyo dhambi amen

23. mimi.ninamkewangu.wandoa.lakini.tunaishi.kama.mtunadadayake.tumezawatoto.wawili.mkubwayuko.kidatochasita.tunaishizaidi.yamiaka.mitatu.hatushirikitendo.landoa.anadai.yeye.ajisikimnisaidie.nikiowa.nitafanya.makosa.

24. Mungu aguse roho za washiriki wa kinondoni wahudhurie effort inayoanza leo biafra na ampatie afya na ujumbe mzito mch tuvako anaeendesha hii.

25. Mungu awabariki.mniombee shetani analeta roho ya hasira kwenye ndoa yetu

26. Mungu naomba unisaidie nipate kazi Crdb..naomba unisaidie kama mchumba huyu ndiye mapenz yako yatimizwe nikifanye maamuz haraka na yasiyo na maumiv kwa yeyote..pia mniombee baba yangu aache pombe kwan amepitiliza na kama familia tunaumizwa sana..AMEN.

27. naitwa Leah, naomba mniombee niishi kwa amani na watu wote,pia naomba Mungu nipate kazi ambayo nimeshafanya interview. Amina

28. NAITWA UPENDO NINANDOA YA MIAKA KUMI NA TATU. NAOMBA MNIOMBEE NIPATE WATOTO NDILO HITAJI LANGU KUBWA KWA SASA.

29. NAMSHUKURU MUNGU KWAMAOMBI YENU YAJUMAPILI NIMEANZA KUPATA AMANI.NIOMBEENI SINA KAZI.MUNGU ANIBARIKI NIPATE KAZI.NIMEMALIZA CHUO MWAKAJANA.PIA NIWE NA AMANI.


30. NAOMBA MAOMBI KWA AJILI YA WATOTO WANGU CHED NA PAULO WAMETUMA MAOMBI YA KAZI HAWAJAPATA

31. Naomba maombi yenu ninasumbuliwa kifua.

32. Naomba mmuombee Ben anafanya mitihani ya taifa leo. Mungu afungue fahamu zake.amina


33. Naomba mniombee mdogo wangu amepata chuo lakin ada haijatosha. Mbarikiwe sana.

34. NAOMBA MNIOMBEE MTOTO WANGU MNDEWA AACHE POMBE ARUD4 KWA MUNGU AENDE KANISANI NI MAMA MNDEWA

35. Naomba mniombee nimechukuliwa nguo ya ndani ikiwa imechafuka na hedhi –

36. Naomba muniombee mungu anijengee nyumba ya kuishi'

37. Naomba mwombee rafiki yangu Lugwisha Ngofilo ili aache pombe,na Mungu amsaidie kuijua kweli na aifuate hiyo kweli.

38. Naomba nione ndoa yangu.ni moses mzakwe wa kimara.

39. Naomba tumwombee yatima huyu aache pombe amekuwa mlevi kupindukia. na mungu amwepushe na marafiki wabaya

40. NAOMBAUMUOMBEE BABA DOMINIKI AMEPARALAIZI AMELAZWA MUHIMBILI AMINA

41. Nataka kuja hapo ofisin kwa maombi na ushauri nijlishe utaratibu tafadhali.

42. Nilimsubili kwa mda wamiaka minne amalize masomo na bado hajamaliza mwaka kesho anamaliza. Leo ananiambia haki kuniowa. Mchungaji naomba uniombe. Kilasiku wazi Wananisema kwa nini hauolewi ? Mimi nawajibu ninamchu yuko chuo .ANAITWA CHALESS. LEO HANITAKI. MIMI NAITWA AGRIPINA NAOMBA UNIOMBEE ILI TUOANE.

43. Nimefungua ofisi ya fenicha .Naomba muiombee . Bwana ailinde. Na aibaliki.

44. Niombeeni jaman, nilikuwa na mchumba. Matokeo yake akanipa mimba na kuniacha sasa nimejifungua namlea mtoto peke yangu! Kwakweli napata maumivu makali kiasi ambacho

45. naweza yanaweza kuniua ghafla na kumuacha mtoto wangu! Niombeeni maumivu haya yaishe pia mungu anibariki ili niweze kumlea mtoto wangu.

46. Niombeeni naumwa ninatumia dawa bila mafanikio


47. NIOMBEENI NIPATE KUOLEWA, NIOMBEENI NIPONE MBA.

48. Tuendelee kuombea nchi yetu iwe na amani. Rais apate safu ya viongozi wazuri. Phillip

49. watu wamungu mniombee kifua kinauma na kuna kunakitu kimekwama kooni

Ikiwa una maoni, ushauri ama hitaji la kiroho usisite kutujulisha.
Sema nasi kwa namba ifuatayo: +255 22 278 0 680.

Maoni 1 :

  1. Mungu azidi kuwabariki wale woote mnaojitoa kwa ajili ya injili.

    JibuFuta