Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Machi 04, 2008

Mugabe apitisha sheria mpya


Vyombo vya habari vya serikali nchini Zimbabwe vimesema kuwa Rais Robert Mugabe amekubali kupitisha sheria mpya ya kuwarudushia wazimbabwe weusi uwezo wa kuwa na dau kubwa zaidi katika makampuni ya umma na yale yanoyomilikiwa na mataifa ya nje.

Sheria hiyo mpya imekuja wiki 3 kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo kufanyika ambapo Bw. Mugabe anachuana na mpinzani mkongwe Bw. Morgan Tsvangirai na aliyekuwa waziri wa fedha Bw. Simba Makoni.

Bw. Mugabe amesema kuwa sheria hiyo itasaidia kuwapa uwezo mkubwa zaidi wa kiuchumi wazawa wa kizimbabwe japokuwa wanompinga wanasema kuwa hatua hiyo itaongeza matatizo ya kiuchumi nchini humo.

Taarifa zinasema kuwa makampuni yatakayoathirika na sheria hiyo mpya ni pamoja na kampuni kubwa sana ya madini Rio Tinto na benki ya Barclays.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni