Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Februari 17, 2008

THE FINAL TRUMPET


Haikuwa rahisi,
ingawa ilibidi iwe sawa na ilivyopangwa.

Hawa washkaji ndio wanaounda kundi hili,
dhamira yao ni kupeleka injili kwa njia ya uimbaji. Tangu mwanzo wao mpaka katika toleo hili la kwanza,maisha yamekuwa na sura mpya.
Jaribu kufanya kile moyo ulichotamani tangu ulipoanza.


Safari yao ya uimbaji wa muziki aina ya Acappella ilileta hamasa kwa vijana na wakaamka.
Ngoja nikudokezee majina yao kwa kila mmoja.


Nikianza na anaye onekana kuanzia kushoto kwako anaitwa ABIHUDI CHIKIRA. Anaemfuatia alieinua mkono wa kushoto ni Mtayarishaji na pia ni Mtangazaji wa Morning Star fm inayopatikana Dar es salaam Tanzania ktk Frequence 105.3 YUSUPH MCHARIA ("Dj Cartoon").

Mwenye shati lenye rangi nyeusi anaitwa MANASE RUSAKA nae ni miongoni mwa watangazaji wa Morning Star fm. Anaehitimisha safuu hii mwisho kulia kwako anaitwa MATHEWS SINGO.

Vijana hawa ukiwaona hakika wanadhihirisha kile MUNGU wanaemtumikia alichowapatia.
Jitahidi upate CD yao wanapatikana katika kanisa la Waadventista Wasabato Kinondoni jijini Dar es salaam Tanzania.

Maoni 1 :