Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Oktoba 19, 2010

KUPATA MORNING STAR RADIO FM

KUTUPATA KWA HOPE CHANNEL INTERTAIONAL
Big Satelite Dishes freq,04070 symbol rate 03003 vertical polrity 2/3.
Small Satelite Dishes freq,26657 vertical polrity 7-10,all frm intelsat Satelite located 68.5 degree east

Jumamosi, Oktoba 16, 2010

MAPANGO YA AMONI

MAPANGO YA AMBONI

Mapango ya Amboni yako katika eneo la Kiamoni, kata ya kiamoni, tarafa ya chumbageni, wilaya ya tanga, mkoa wa tanga. Ni eneo zuri la kupumzikia, kwa tafi za kihistoria, kijiografia, kijiolojia, n.k


Mapango haya yako umbali wa kilomita 8 toka tanga mjini kupitia barabara kuu inayoelekea Mombasa. Unaweza kufika katika hifadhi ya mapango kwa kupitia mojawapo ya njia zinazoelekea huko. Ya kwanza ni barabara ya changarawe iliyo upande wa kushoto meta 200 baada ya kuvuka daraja la hofu, ya pili iko kilometa 1.5 kutoka daraja la utofu katika kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu. Njia zote zinapitia katikati ya kijiji cha kiamoni.


Mapango haya yametokana na mabadiliko ya nguvu za asili zilizobadilisha maumbile ya miamba ya chokaa kipindi cha jurasiki (Jurassic period) kama miaka inayosadikiwa kuwa zaidi ya milioni 150 iliyopita. Kulingana na tafiti zilizokwishafanywa, eneo hili la mapango lilikuwwa tena chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita na linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 234 lenye mazingira ya miamba ya chokaa. Ni eneo ambalo linapitiwa na mito na limejaa uoto wa asili.


Miamba ya chokaaa kwa asili huundwa na madini ya kashiamu kabonate [ Calcium carbonate=CaCo3]. Miamba hii ni migumu kumomonyolewa na maji ya kawaida, lakini ni rahisi kuyeyushwa na maji yenye kiasi kidogo cha tindikali ya kaboni (Carbonic Acid). Tindikali ya kaboni iliyobadilisha maumbile ya miamba hii kwa kumomonyoa na kusababisha mapango yaweza kutokana na maji ya mvua yanapochanganyika na dioksidi ya kaboni (carbodioxide) hewani kabla ya kufika ardhini au na dioksidi ya kaboni inayopatikana ardhini. Maji yanapojipenyeza ardhini huendelea kupokea dioksidi ya kaboni kutoka muozo wa viumbe hai kama mimea na wanyama na kutengeneza tindikali. Tindikali ya kaboni inapopambana na madini ya kashiamu kaboneti (calcium carbonate) katika miamba ya chokaa husababisha kumomonyoka kwa miamba hii katika maeneo mbalimbali na kusababisha mapango. Mabadiliko haya huitwa kabonesheni (carbonation). Angalia mchanganuo wa kemikali ufuatao.


Wataalam wanaelezea njia mbalimbali zilizosababisha mapango katika eneo hili.


Kulingana na utafiti uliofanywa na mturi (1979), njia ya kwanza ni ile ya maji ya mvua yanapochanganyika na hewa ya “Carbondioxide” katika anga na kutengeneza tindikali (carbonic acid) ambayo inauwezo wa kuyeyusha madini ya calcium carbonate yanaunda sehemu kubwa ya miamba ya chokaa. Maji haya yenye tindikali husababisha mabadiliko kidogo yanapotelemka kuelekea ardhini. Yakifikia meza ya maji (water table) huku yakiendelea kuongezeka huzidi kuchanganyika na carbondioxide) iliyoko kwenye maji ardhini.


Kina cha maji kikiongezeka maji haya yenye tindikali huwa na uwezo wa kuyeyusha maungio ya miamba katika sehemu laini zaidi za miamba na kusababisha nyufa. Nyufa hizi huzidi kupanuliwa na maji yanayotembea na kusababisha baadhi ya mawe kuporomoka na kufanya mapango. Kasi ya maji inapozidi njia ndogondogo hupanuliwa na kuwa kubwa zaidi na upo uwezekano mapango madogo madogo hupanuliwa na kuwa kubwa zaidi na upo uwezekano mapango madogo madogo kuunganishwa na hatimaye kuwa na mfululizo wa mapango kama yanavyoonekana katika eneo hili.


Kina cha maji kinapopungua eneo huachwa likiwa kavu, lakini mabadiliko hayo huweza kuendelea kutokea chini zaidi na kusababisha njia na mapango mengine katika kina kingine ambapo hutokea muunganiko wa mapango kwa baadhi ya maeneo.


Njia nyingine ni pale ambapo inasemekana eneo hili lilikuwa chini ya usawa wa bahari yaani pembeni ya ufuko wa bahari. Mawimbi ya bahari yakamomonyoa miamba ya chokaa na kusababisha mapango. Baada ya bahari kurudi nyuma kutokana na kupungua kwa kina chake katika eneo hili, eneo la mapango likaachwa likiwa kavu.


Njia zote zilizoelezwa zimehusika katika kutokea kwa mapango haya, Mapango ya kwanza yatakuwa yalitokana na mmomonyoko wa miamba ya chokaa kutoka na maji ya ardhini yenye tindikali yaliyoyeyusha maungio ya miamba ya chokaa na kusababisha mapango. Kina cha bahari kilipopanda, maji ya bahari yalifikia eneo la mapango na mawimbi yake kusababisha kupanuliwa kwa mapango au mabadiliko katika kuta za nje na ndani ya mapango. Kina cha bahari kiliposhuka, eneo la mapango kilikuwa chini sana, maji ya mvua yenye tindikali yamekuwa na uwezo wa kuendelea kupanua na kubadilisha mfumo wa mapango.


Haijulikani mapango haya yaligunduliwa lini, bali taarifa zilizopo zinaonesha kwamba watu wa makabila yaliyoishi jirani na eneo la mapango: Wabondei, Wasambaa, Wadigo, na Wasegeju wamekuwa wakiya tumia kwa ajili ya matambiko ya mizimu tangu karne ya 16. Eneo hili la mapango kwa wakati huo lilijulikana kama eneo la mzimu wa mabavu.


Watu wanaamini habari za nguvu za mizimu katika kutatua matatizo ya uzazi, kuongeza kipato, magonjwa n.k. Kwa hivi sasa hutoka sehemu mbali mbali za Afrika Mashariki na kuja kuomba au kutambikia mizimu katika vijipango mbali mbali. Mbali na matumizi hayo, kampuni ya kigeni iliyojulikana kama “Amboni Limited” ilimiliki mashamba ya mkonge katika eneo la ta nga na kuweka eneo hili chini ya himaya yake mwaka 1892 ili kulitumia kama sehemu ya kupumzikia. Hii inatokana na mazingira mazuri na yenye utulivu ya mapango ya Amboni. Baadaye kampuni hii ilijulisha serikali kuhusu kuwepo kwa mapango haya. Serikali ilichukua hatua kutangaza eneo la mapango kuwa eneo la hifadhi mwaka 1922.


Mwaka 1937 ilipitishwa sheria ya mambo ya kale (Monuments Preservation Ordinace of 1937) iliyofuatiwa na ile ya 1953 (Monuments Preservation Ordinace of 1953) ambayo ingesaidia kulinda mambo ya kale ikiwa ni pamoja na mapango ya amboni. Mwaka 1963 serikali ya Tanganyika ikayaweka mapango chini ya usimamizi wa idara ya mambo ya kale. Mwaka 1964 serikali ilisimamisha sheria ya kikoloni ya 1937 na 1953 na kupitisha sheria ya mambo ya kale ya mwaka huo (The Antiquities Act of 1964) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1979 (Amendments Acts of 1979) kwa ajili ya kulinda mambo ya kale nchini. Kwa upande wa mapango ya Amboni, mbali na mambo mengine sheria inakataza kuandika au kuchora kwenye kuta za mapango.

VIVUTIO:



  1. Kuna maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kuomba au kutambikia mizimu ambapo utaona vitu vingi vinavyohusiana na imani za kijadi.

  2. Kuna miamba yenye maumbo ya kuvutia yanayofanana na Sofa/Kochi, Meli, Mamba, Tembo, Sanamu ya bikira maria n.k. Kuna vitu vinavyoonekana kama michoro inayofanana na unyayo wa mguu wa binadamu, na mnyama inayotokana na uchafu, hasa vumbi na udongo ambao hunywea pamoja na maji ya mvua na hatimaye kuganda katika paa la pango. Alama nyingine ni zile zilizosababishwa na popo wanaoishi mapangoni.

  3. Kuna miamba inayokua au kuongezeka (Speleothems/Dripstones) kutokana na mabadiliko ya kikemikali katika miamba ya chokaa. Mabadiliko haya hutokana na maji yenye tindikali kuyeyusha madini ya “Calicium Carbonate”, kuyahamisha na kuya rundika katika eneo jingine. Mtokeo ni kupata miamba inayokuwa kutoka juu kuelekea chini (stalactite) au inayoelekea juu (stalagmite). Kulingana na utafiti uliofanywa na Mapunda na Msemwa (2005:101). Miamba ya aina hii huongezeka/kukua kwa kasi zaidi kipindi cha mvua kuliko kipindi cha kiangazi. Katika miaka kumi iliyopita, ukuaji wa miamba ya aina hii ni milimeta 0.5 kila baada ya miaka 100. Na kwamba iliwahi kuongezeka kwa kasi ya milimeta 7 katika kila miaka 100 kipindi cha kati ya miaka 38,000 na 34,000 (38 & 34 Ka)


Yapo masimulizi mengine yanayohusu mapango haya, mfano:


Kuna simulizi zinazoelezea njia za mapango zinazoelekea Mombasa, Maweni, Mkoa wa Kilimanjaro n.k. Vile vile zipo simulizi za Osale Otango (Samuel Otango) na (Paulo Hamis). Watu hawa waliwahi kutumia kituo namba tatu ndani ya pango kubwa kama sehemu yao ya kujificha kati ya mwaka 1952 na 1956 huku wakiendesha harakati za kupambana na walowezi waliokuwa wamewekeza katika maeneo ya Tanga. Walipora mali na kutishia maisha ya walowezi katika maeneo mbalimbali. Serikali ya kikoloni iliwatambua kama wahalifu na kujaribu kuwakamata bila mafanikio kwa kipindi kirefu. Mwaka 1957 Paulo Hamis alipigwa risasi maeneo ya Lushoto na kufariki. Wananchi wa kawaida wanawakumbuka kama mashujaa walioendesha harakati za ukombozi wa watu wanyonge kutoka katika mikono ya walowezi na watawala wa kikoloni.


NUKUU:


Habari hizi zimeandikwa kutokana na masimulizi pia maelezo kutoka katika vitabu mbalimbali:-


1. Institute of Curriculum Development: Geography Coourse Book for Secondary Schools Book 3.


2. Lutgens, F.K and Edward J.Tartbuck (2000). Essentials of GEOLOGY. SEVENTH EDITION. Upper Saddle River, New Jersey: Printice-Hall, Inc.


3. Mapunda, B.B.B and Paulo Msemwa (2005). Slavaging Tanzania’s culture Heritage, Dar es Salaam. Dar es Salaam University Press.


4. Mturi, A.A (1998). Archeology of Tanzania, Dar es Salaam: The Open University of Tanzania.


5. Mturi, A.A (1975). A guide to Tongoni Ruins, Dar es Salaam.


Ama, unaweza kupata maelezo zaidi kwa kuwasiliana kupitia mawasiliano haya:


Mapango ya Amboni.
S.L.P 5028,
TANGA.

Simu: +255 784 788 990 na +255 784 546 302.

Ijumaa, Oktoba 15, 2010

HAMU HAIISHI LEO

NI MWANZO MGUMU LAKINI WENYE NEEMA, SIKU YA KULA MAZIWA NA ASALI. UNAWEZA DHANI NI SUALA LA KUFIKIRIKA LAKINI NI ZAIDI YA KIKOMO CHA MAWAZO NA FIKRA ZETU ZINAPOISHIA. SASA, TARAJIA ZAIDI MAANA MWENENDO WETU UNATULETEA MAMBO MAGUMU NA KUYAFANYA MAISHA KUWA KITU KISICHO MUHIMU NDIO MAANA LEO MWANAMKE AMA MWANAMME YUPO RADHI ASIKUPE RUHUSA YA KUCHEZEA AMA KUTUMIA GARI LAKE LINALOTUMIA MAFUTA IWE NI DIESEL AMA PETROL LAKINI MWILI UNAWEZA KUUFANYIA CHOCHOTE ILIMRADI ETI UNAITULIZA TAMAA!!! HAMU HAIISHI JAMANI.