Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Juni 30, 2013

VIFAA VYA KUTUNZIA KUMBUKUMBKUMBU NJE YA KOMPYUTA VIJULIKANAVYO KAMA REMOVABLE DEVICES.


Kama ilivyo kwa mashine kadhaa na vyombo mbalimbali, kompyuta inaweza kupata hitilafu na hatimaye kupoteza kumbukumbu muhimu sana katika maisha ya kawaida ya jamii. Hivyo panapaswa kuwa na njia mbadala ya kutunza kumbukumbu pindi ikitokea tatizo kama hilo. Kuna vifaa maalum vya kutunzia kumbukumbu ambazo ni muhimu mno. Vifaa hivi huweza kuingizwa katika kompyuta, kuchukua kumbukumbu na kuvitoa kwenda kuvihifadhi mahali ambako ni salama zaidi. Vifaa hivi vinafahamika kama storage devices. Kwa sababu vifaa hivi huweza kutolewa ndani ya system case ya kompyuta hufahamika pia kama removable devices.

Vifaa hivi huingizwa katika Kompyuta kwa kupitia matundu maalum yafahamikayo kama ports na milango maalum ifahamikayo kama drivers. Vyote hivi hujengwa katika system case na huonekana sehemu ya mbele na ama sehemu ya nyuma ya system case.
System case ikiwa na milango na tundu vifahamikavyo kama drivers na port

CD ni nini?

Hiki ni kifaa cha kutunzia kumbukumbu na ambacho kinaonekana kuwa kama kimekuwa mbadala
wa tapes zilizozoeleka kwa muda mrefu katika utunzaji wa muziki na habari mbalimbali. Ni kifaa
ambacho kinatunza kumbukumbu za aina zote; ikiwa na maana text (maneno na picha), sauti na
video. Kifaa hiki kina umbo bapa la mviringo na kina sehemu iliyo kama kioo ambako habari na
data huwekwa. Bila shaka umekwisha kutana na kifaa hiki katika maisha ya kila siku.
 
Picha ya CD

CD ni kifupi cha maneno Compact Disc. Disc hii imetengenezwa kuhifadhi habari na data katika mfumo wa digital, teknolojia mpya ya kuhifadhi kumbukumbu ambayo imeiweka kando teknolojia ya zamani iliyofahamika kama analogue. Kwa mfano mikanda ya muziki na filamu ambayo ilikuwa na mkanda ulioviringishwa katika kifaa kilichoweza kuzunguka na hatimaye kutoa sauti ama kuonesha picha (tazama picha hapa chini) ilikuwa imeundwa kutumia teknolojia ya analogue.      
VHS tapes

CD huingizwa katika kompyuta ili kuwekewa ama kuingiza data na habari katika kompyuta.Kitendo cha kupeleka data na habari kwenye kompyuta hufanywa na kifaa maalum kilicho namlango ambao hufunguka na kufunga na ambao unaweza kubeba CD. Kifaa hiki hufahamika kama CD driver. Mlango huu huwa na taa yenye rangi ya njano-kijani ambayo huwaka pindi CDinapokuwa imewekwa na inafanya kazi ya kusoma data na habari. Kwa kawaida utasikia sauti ya CD kuzunguka katika CD driver. CD driver hufanya kazi ya kuiwezesha kompyuta kuitambua CD na kuifanya ipeleke data au kutoa data. Kazi hii ya kupeleka data au kuifanya kompyuta ipokee habari na data kutoka kwenye CD huitwa reading ama kusoma kwa kiswahili. Kama mtu anakwambia kompyuta inasoma data au habari zilizo katika CD anakuwa anamaanisha kuwa kompyuta hiyo inahamisha data kutoka kwenye CD kwenda katika sehemu ambayo huwezesha data kuonekana kwenye monitor, sehemu ambayo hufahamika kama random access memory

(RAM). Pia kitendo cha kuhamisha data kutoka kwenye kompyuta (yaani hard disk) kwenda kwenye CD hufahamika kama writing ama kuandika. Kitendo cha kuandika habari na data katika CD kutoka mahali zilipohifadhiwa (hard disk) kinawezekana tu kama CD driver ambako CD hiyo huwapo inaweza kuandika habari na data kama itakavyoelezwa hapo baadaye.

Kwa kawaida CD ina uwezo wa kuhifadhi habari ama data zenye ukubwa wa MB 700. Kwa hiyo Kama una habari ama data zenye ukubwa huo na unataka kuzihamishia kwenye kompyuta basi utakuwa unahamisha MB 700 na kama unataka kuzihamisha kutoka hard disk kwenda CD basi utakuwa unahamisha MB 700. Kwa kawaida software nyingi huja zikiwa zimehifadhiwa ndani yaCD na huingizwa katika kompyuta kwa njia ya hizi. Kwa mfano Kama tulivyo sema software mamayaani OS hutakiwa kuingizwa katika hard ware part ya kompyuta ili kuifanya kompyuta ifanyekazi. Software hii huwa ndani ya CD. Kitendo cha kuingiza software ndani ya kompyuta kupitia
CD hujulikana kama installation. Kuna hatua za kufuata katika kufanya kitendo hiki na mara nyingi ni wataalam wa masuala ya kompyuta wanafanya kazi hii. CD pia huhifadhi habari mbalimbali kama muziki, picha za video na za kawaida na data za aina nyingine.

 
Kuna aina kadhaa za CD kulingana na teknolojia ya kuzitengeneza

CD kwa kawaida zimegawanyika katika makundi kadhaa

DVD – aina ya CD yrnyr uwezo mkubewa wa kuhifadhi habari na Data

DVD ni kifupisho cha maneno Digital Versatail Disc. Ni aina ya CD ambao ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi data na habari na hakika ni kutokana na uvumbuzi wa kifaa hiki kumeweza kuwa na ubebaji wa data au habari nyingi kwa wakati mmoja. Kifaa hiki kinafanana kabisa kabisa na CD ya kawaida kimuonekano. Tofauti yake na CD ya kawaida ni teknolojia iliyotumika katika utengenezaji. Kwa kawaida CD hutengenezwa ikiwa na sehemu ndogondogo zijulikanazo kama tracks. Tracks hizi huwa katika mpangilio maalum wa mviringo. Kwa sababu CD ni ya Duara, kuna duara nyingi zilizobeba tracks zinazofahamika kama sectors. Data au habari hutunzwa katika kila track ambazo kusanyiko wa tracks huzaa sectors.

Utengenezaji wa CD hutofautiana na ule wa DVD kutokana na mpangilio wa sectors na tracks. Katika DVD kuna tracks nyingi katika sector moja kuliko katika CD ya kawaida. Kwa namna nyingine tunaweza kusema kuwa DVD ina sector nyingi kuliko CD. Kwa namna hii DVD inakuwa na uwezo wa kubeba data nyingi sana kuliko CD. Tuliona kuwa CD ina uwezo wa kubeba data katika uwezo wa kikomo cha MB 700. Hii ni tofauti kwa DVD ambayo ina uwezo wa kubeba data mpaka mara saba zaidi ya ile ya CD. DVD inaweza kubeba data au habari mpaka kufukia MB5000 au GB 5. Ni kwa namna hii ndiyo maana watengenezaji wa filamu na muziki hupenda
kuhifadhi filamu zaidi ya moja (mpaka kufikia 20) katika DVD.

Kama CD pia DVD inaweza kuwa tupu na ukahifadhi data au habari kwa kutumia kompyuta. Hizihuwa zinakuwa katika mfumo wa kuweza kuandikwa. Kuna DVD – R na DVD – RW. DVD – R inasimama badala ya DVD – Recordable ikiwa na maana kuwa unaweza kuhifadhi data kwa kuiandika (writing) mara moja pekee na baada ya hapo inakuwa DVD ya kawaida (yaani ya kusoma tu). DVD – RW inasimama badala ya DVD – Rewritable ikiwa na maana kuwa ina uwezo wa kuhifadhi data au habari zaidi ya mara moja; ikiwa na maana kwamba unaweza kuhifadhi data ukazifuta na kuweka nyingine tena. Hata hivyo kuna ukomo wa kuandika data katika DVD ambapo
inakuwa haina uwezo tena wa kufutwa.

Ili uweze kutumia DVD katika kompyuta inakubidi uwe na DVD river. Hii ni tofauti na DC driver ambayo huwezesha CD kutambulika katika kompyuta. DVD driver imetengenezwa katika tekonlojia ambayo inawezesha kusoma DVD. Kwa kawaida DVD driver huwekwa ktika system case mahali ambako CD driver huwekwa na kuunganisishwa na mothreboard kwa kutumia nyaya zilezile zitumikazo kuunganishia CD driver.

System case ya kompyuta huwa na milango zaidi ya mmoja (inaweza kufikia mitatu) inayowezesha drivers kufungwa na kuunganishwa na motherboard. DVD driver inaweza kuwekwa katika mlango ambao CD driver inatumia. Hata hivyo habari nzuri ni kwamba teknolojia iliyotumika kutengenezea CD driver iitangulia kabla ya ile ya kutengenezea DVD driver, hali inayoifanya DVD driver kuweza kusoma (kutambua) CD na DVDs. Kwa maana hiyo ukiwa na DVD driver katika kompyuta unakuwa na uwezo wa kutumia CD na DVD. DVD driver huwa zimeandikwa DVD ROM au DVD RW katika milango ya kupachika CD au DVD na CD driver huwa zimeandikwa CD ROM au CD RW katika mlango wa kuwekea CD. 

CD & DVD Driver



CD na DVD huweza kutunza data na kumbukumbu kwa muda ambao hutegemea na utunzaji wake. Kwa kawaida CD au DVD huwa na tundu katikati ambalo hutumika kama kishikio

kinachomwezesha mtumiaji kutogusa sehemu ya nyuma ambayo huonekana iking’aa na inayoweza kuonesha taswira mathalani ya uso wa mtu. Sehemu hii ndiyo huwa na data. Kama sehemu hii ikiguswa na uchafu mathalan vumbi na mafuta kutoka mikono ya mtumiaji inaweza kusababisha data kutotumika vyema. Athari ya uchafu katika CD au DVD huonekana mara unapoingiza katika driver ya kompyuta. Haitakuwa inazunguka vyema na itakuwa inakwama kila mara na hii hatimaye hufanya data kutosomeka vyema au kupotea kabisa.

Kwa kawaida CD na DVD huwa zimehfadhiwa katika mifuko laini ya nailoni ambayo huzuia vumbi na uchafu mwingine. Kwa maana hiyo unapotumia CD au DVD inakupasa kuhakikisha kuwa unaiihifadhi vyema katika mifuko ya nailoni na hakikisha kuwa haugusi sehemu zinazong’aa. Kama utahakikisha kuwa unafanya matunzo mazuri basi CD au DVD kitakuwa chombo kizuri cha kuhifadhi data.

Floppy Disk - Kifaa cha kwanza kutunzia na kuhamisha habari au Data katika
Kompyuta

Floppy Disk ni kifaa chenye umbo la penbe nne kama msitatili hivi ambacho kwa muda mrfu kiliyumika kuhifadhi data au kuhamisha data kutoka kompyuta moja kwenda nyingine. Kifaa hiki kina sehemu ndogo laini yenye umbo la mviringo ambayo kwa kawaida huwa imefichwa katika sehemu ngumu ya nyuma na ya mbele. Sehemu ya mbele inaweza kusukumwa mbele na nyuma ili kuwezesha data au habari kuandikwa na kusomwa na kompyuta ndani ya driver ifahamikayo kama floppy driver. Floppy Disk ni tofauti kabisa na Cd au DVD katika ubebaji wa kumbukumbu na data kwani inatumia teknolojia tofauti.







Tofauti na CD au DVD drivers, Floppy driver haina mlango ambao unaweza kufunguka na kufungwa badala yake huwa na tundu dogo la pembe nne ambalo huwezesha floppy disk kuchomekwa kwa kusukuma ndani taratibu. Floppy disk hutolewa ndani ya kompyuta kwa kubonyeza kitufe kidogo kilicho pembeni ya tundu la kuuingizia. Kuna aina mbili za floppy disk drivers, ile ambayo inakuwa kama sehemu ya system case ya kompyuta kama inavyoonekana katika picha A hapo juu na ile ambayo inaweza kuungwa katika kompyuta kwa kutumia waya wa
kuingiza na kutoa data (cable) ifahamikayo kama external floppy driver picha B hapo juu.

Floppy disk inaonekana kutotumika katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu teknolojia yake inaonekana kupitwa na wakati. Hii inachangiwa na ukweli kwamba ina uwezo mdogo wa kuhifadi data na kumbukumbu. Ina uwezo wa kubeba na kuhifadhi data na habari zenye ukubwa wa MB 1.35 tu. Hii inaifanya kuweza kubeba habari na data zenye ukubwa mdogo sana ambazo mara nyingi ni maandishi (text files). Kumbuka kuwa kiwango hiki kinazidiwa na DVD kwa zaidi ya mara 5000!

Zip Disk – kifaa cha kutunzia na kubebea kumbukumbu kinachofananishwa
na CD

Kabla ya uzinduzi wa CD palikuwa na kifaa ambacho kiliweza kubeba data na kumbukumbu kwa kiasi kikubwa kama kile cha CD ya kawaida. Kifaa hiki hufahamika kama Zip Disk. Kina umbo sawa na lile la Floppy disk. Ni kifaa ambacho kina uwezo wa kuhifadhi data na kumbukumbu zenye kufikia kiwango cha MB 700. hata hivyo kifaa hiki kinaonekana kutotumika tena na ni wachache sana ambao wanakitumia ni nadra kukuta kompyuta za kisasa zikiwa na Zip Driver, driver ya kuwezesha kompyuta kuitambua Zip Disk.

Hata hivyo system case nyingi za kisasa huwa na CD au DVD driver pamoja na Flopp Driver
pekee.

Memory Stick almaarufu Kama Flash Disk

Hiki ni kifaa ambacho kinatumika sasa katika miaka ya hivi karibuni katika ubebaji na uhfadhi wa data. Ni kifaa kidogo ambacho kinaweza kulingana na kidole gumba cha mtu mzima. Memory stick kinafahamika sana kama Flash Disk kwa watumiaji wengi wa kompyuta na kinaundwa katika maumbo na mtindo mbalimbali. Kinafahamika kama Flash Disk kwa sababu data zake au kumbukumbu zinazohifadhiwa zinaweza kufutwa na kuandikwa kwa muda mfupi na mara nyingi kuliko kifaa kingine kinachoitwa removable storage device. Kifaa hiki kinatofautiana ukubwa wa kuhifadhi data tofauti na vifaaa vingine tulivoviona hapo juu. Memory stick huwa na ukubwa unaoanzia MB 128 mpaka GB zaidi ya 10. Ni kifaa ambacho kinapendwa na watu katika kuhifadhia kumbukumbu kwa sababi ni kidogo kwa umbo na kinaweza kubebwa kwa urahisi hata katika mfuko wa suruali.

Memory stick huwasiliana na kompyuta kupitia matundu maalum yajulikanayo kama (USB ports) Universal serial Bus ports. Haya ni matundu ambayo huwa nyuma na ama mbele ya system case ya kompyuta. Kwa kawaida matundu haya hutumika pia kwa kupachika vifaa kama Mouse, Camera na printers. Memory stick huandikwa ukubwa ilio nao katika sehemu ya nje. Unaweza kukuta memory stick ya kampuni ya Sony ikiwa na MB 512, kwa mfano.

Memory sticks zinatunika sana sasa katika uhamishaji na ukusanyaji wa data na habari na kuhamisha kati ya kompyuta moja na nyingine. Tutaona baadaye madhara ya matumizi ya CD, DVD, Floppy Disk, na Memory stick katika kompyuta.

Memory stick kama vilivyo vifaa vingi vya kielektroniki, imeundwa kwa kutumia muunganiko wa sakiti ndogo ambayo huwa imehifadiwa ndani ya material aina ya plastiki. Unapoishika flash disk unakuwa unaona umbo au material haya ya nje tu ambayo ndani yanakuwa yamehifadhi sakiti inayohifadhi data au habari. Sakiti hii huwa na sehemu iliyotokeza nje ambayo hapa tunaweza kuiita mdomo ambao ndio huingizwa katika tundu la kompyuta (USB port).

Removable devices zina umri wa kuishi!

Kwa kawaida CD, Floppy disk, DVD, na vifaa vinginevyo vya kuhifadhiwa ambavyo vinabuniwa kila kukicha vina muda maalum wa kuhifadhi kumbukumbu. Baada ya muda fulani ambao hutegemea na utunzaji wa kifaa husika kifaa hicho kinakuwa hakina uwezo tena wa kuhifadhi kumbukumbu hizo. Kuna sababu kadhaa ambazo zinafanya vifaa hivi kuishiwa na ama kukosa kabisa uwezo wa kuhifadi tena kumbukumbu. Zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo:

Uchafu

Hapa inamaanisha hasa vumbi katika vifaa hivi. Kwa kawaida vifaa kama CD na Floppy Disk huwa na sehemu ambayo huakisi mwanga ambao ndio hufanya kazi ya kutafsiri data na habari. Sehemu hizi kwa kawaida hutakiwa kuwa safi kabisa. Endapo itatokea vumbi na chembechembe zozote za uchafu zikakutana na sehemu hizi basi kumbukumbu zilizohifadhiwa juwakatika hatari ya kupotea. Na mara nyingi dalili ya kutofanya kazi kwa ufanisi ni kukwama-kwama kwa CD au kuchukua muda mrefu kufunguka kwa floppy disk pindi zinapokuwa katika drivers. Hali hii hatimaye husdababisha kompyuta kutosoma kabisa kumbukumbu hizi. Na ndiyo maana watengenezaji wa CD huziweka katika makasha na vifuko maalum ambavyo huzuia vumbi na vitu vingine kuingia katika sehemu ya nyuma ambayo ukiitazama vyema utagundua kuwa ni kama kioo. Pia floppy disk huiifadhi sehemu ya kusoma data ndani ya plastiki ngumu ambayo hufunguka na kubaki wazi pindi inapoingizwa kwenye floppy driver.

Plastiki ama aluminium ambayo huhifadhi sehemu ya kusoma data ambayo hubaki wazi pindi inapoingizwa kwenye kompyuta

Maji ama unyevu

Haya huweza athiri vifaa fivi kwa maana kwamba pindi yanapoingia katika vifaa g